Dollar

38,2552

0.34 %

Euro

43,8333

0.15 %

Gram Gold

4.076,2000

0.31 %

Quarter Gold

6.772,5700

0.78 %

Silver

39,9100

0.36 %

Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele amesema kuwa wao kama tume wametafsiri sheria hiyo wanavyojua wao, na iwapo CHADEMA wana tafsiri tofauti ni haki yao, ila waachie uamuzi wa mwisho mahakama.

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kimetaja marufuku ya uchaguzi kuwa ni kinyume cha katiba

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema Jumanne kutenguliwa kwake katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ni kinyume cha katiba, siku chache baada ya kiongozi wake kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.

CHADEMA ilikataa kutia saini hati ya maadili ya uchaguzi, na hivyo kukizuia kushiriki katika uchaguzi wa urais na ubunge unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mosi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilisema Jumamosi.

Kiongozi wa chama, Tundu Lissu, ambaye alinusurika kupigwa risasi 16 mwaka 2017, alishtakiwa kwa uhaini wiki iliyopita kwa kile waendesha mashtaka walisema ni hotuba ya kuwataka wananchi kuanzisha uasi na kuvuruga uchaguzi.

Kwa kumshtaki Lissu kwa kosa la kifo na kukifungia chama chake kushiriki uchaguzi huo huenda serikali ikavutia kuchunguzwa zaidi rekodi yake ya haki.

Mageuzi katika mchakato wa uchaguzi

“Haki ya kikatiba haiwezi kuondolewa kwa kanuni za maadili zilizoundwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema Rugemeleza Nshala, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA. Reuters haikuweza mara moja kumfikia msemaji wa tume ya uchaguzi ili kutoa maoni yake.

Hapo awali CHADEMA ilitishia kususia uchaguzi isipokuwa mageuzi makubwa yatafanywa katika mchakato wa uchaguzi ambayo inasema inapendelea chama tawala.

Hapo awali CHADEMA ilitishia kususia uchaguzi isipokuwa mageuzi makubwa yatafanywa katika mchakato wa uchaguzi ambayo inasema inapendelea chama tawala.

"Msimamo wetu bado ni uleule: hakuna mageuzi, hakuna uchaguzi," Nshala alisema.

INEC yasema uamuzi uachiwe mahakama

Kwa kujibu tamko la CHADEMA, mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele amesema kuwa wao kama tume wametafsiri sheria hiyo wanavyojua wao, na iwapo CHADEMA wana tafsiri tofauti ni haki yao, ila waachie uamuzi wa mwisho Mahakama.

Wanaharakati wa kupigania haki na vyama vya upinzani wameishutumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, wakitaja msururu wa utekaji nyara na mauaji yasiyoelezeka.

Serikali imekanusha madai hayo na imefungua uchunguzi kuhusu utekaji nyara unaoripotiwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#