Sport
Dollar
38,2003
0.25 %Euro
44,2054
1.59 %Gram Gold
4.159,3000
2.02 %Quarter Gold
6.767,1400
0 %Silver
40,2400
0.79 %Joseph Kabila aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka 2001 hadi 2019.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekisimamisha chama cha kisiasa cha Rais wa zamani Joseph Kabila na kuamuru mali zake kuchukuliwa kwa tuhuma za kuwaunga mkono waasi mashariki mwa nchi hiyo, serikali ilisema.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 53, ambaye alitawala kuanzia 2001-2019, amesema anataka kurejea Congo kusaidia kutafuta suluhu la vita.
Lakini katika taarifa mwishoni mwa Jumamosi, wizara ya mambo ya ndani ilisema kuwa chama chake kilisimamishwa kwa kuwasaidia waasi wa M23, huku wizara ya sheria ikisema mali zake na za viongozi wengine wa chama zitakamatwa baada ya vitendo vya uhaini mkubwa.
Taarifa zote mbili zilisema waendesha mashtaka walikuwa wameagizwa kuanzisha kesi dhidi yake, lakini hakuna maelezo ya mashtaka yaliyotolewa.
Mashambulio ya waasi
Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa Kabila.
Ferdinand Kambere, katibu wa Chama chake cha Kujenga Upya na Demokrasia, alitaja kusimamishwa huko kuwa ni ukiukaji wa wazi wa katiba na sheria za Congo, shirika la habari la Reuters linaripoti.
M23 wamechukua miji miwili mikubwa katika eneo la mashariki lenye utajiri wa madini tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Eneo hilo limekumbwa na miongo kadhaa ya migogoro iliyotokana na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na mapambano ya udhibiti wa madini.
Kabila aliingia madarakani baada ya kuuawa kwa baba yake na alikataa kuondoka muda wake wa mwisho ulipokamilika mwaka wa 2016. Hatimaye alikubali kujiuzulu kufuatia maandamano makubwa na ameishi katika mataifa tofauti ya Afrika tangu wakati huo.
Comments
No comments Yet
Comment