Sport
Dollar
38,4292
0.2 %Euro
43,8350
-0.02 %Gram Gold
4.095,0600
-0.84 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Uturuki ameeleza sifa za taifa lake katika suala la michezo duniani wakati wa hafla ya maandalizi ya mechi za Euro 2032.
Rais Recep Tayyip Erdogan amesisitiza utayari wa Uturuki wa kuwa wenyeji wa Michezo ya Olimpiki, akieleza sifa za nchi yake katika kuandaa michezo ya kimataifa na miundombinu yake ya kisasa kabisa.
Alisema hayo siku ya Alhamisi wakati wa ufunguzi wa ofisi mpya za shirikisho la soka barani Ulaya UEFA jijini Istanbul, zilizozinduliwa kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya soka ya UEFA Euro 2032, ambayo Uturuki itakuwa mwenyeji mwenza pamoja na Italia.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi, Erdogan alisema Uturuki imekuwa ikionesha uwezo wake wa kuandaa michezo ya kimataifa na kusisitiza kuwa “ina uwezo wa kutosha kuandaa michezo yoyote ya dunia, ikiwemo Olimpiki.”
Rais alieleza sifa za Uturuki kama nchi yenye uzoefu na ya kutegemewa katika kuandaa michezo hiyo, akieleza kuhusu ushirikiano wa muda mrefu kati ya taifa lake na UEFA na kuchaguliwa kwa Istanbul kwa mechi kubwa kubwa za mpira wa miguu.
Ofisi za UEFA zitaimarisha jukumu la Uturuki bara Ulaya
Uamuzi wa UEFA kufungua ofisi jijini Istanbul ni ishara ya kuongezeka kwa umuhimu wa Uturuki katika soka la bara Ulaya na nafasi yake ya kimkakati katika suala la michezo duniani. Ofisi hiyo itakuwa na jukumu la kuandaa na kuratibu mechi za Euro 2032 ikishirikiana Uturuki na Italia.
Rais Erdogan aliwakumbusha waliohudhuria kuhusu mafanikio ya Uturuki kuandaa mechi kadhaa za UEFA katika miaka ya hivi karibuni.
Hii ikiwa ni pamoja na Fainali ambayo haiwezi kusahaulika ya mwaka 2005 UEFA klabu bingwa Ulaya kati ya Liverpool na AC Milan, ambayo siku zote hutajwa kama mechi isiyosahaulika katika historia ya soka, pamoja na Fainali za Kombe la UEFA 2009, Kombe la UEFA Super Cup 2019, na ya hivi karibuni, Fainali ya UEFA ya Kombe la Klabu bingwa Ulaya 2023.
Dira mpya kuhusu Olimpiki
Kila mchezo, alisema, ni ushahidi tosha wa uwezo wa Uturuki katika kuandaa, miundombinu ya kisasa, na mapenzi yake kwa michezo.
Licha ya kuwa Uturuki haijawahi kuwa wenyeji wa Michezo ya Olimpiki, imejaribu mara kadhaa kuomba kuandaa, hata Olimpiki ya 2020.
Hotuba ya Erdogan inaonekana kama ishara mpya ya kutaka kuomba fursa zingine za kuandaa Olimpiki, akitaja sifa ya nchi yake ya kuwa na miundombinu ya kisasa na uzoefu wa kuandaa michezo ya kimataifa.
Mechi za UEFA Euro 2032, zinazotarajiwa kuandaliwa kwa pamoja na Uturuki na Italia, ni ishara ya hatua kubwa kwa nchi baada ya mara nyingi kujaribu kuomba uwenyeji wakiwa peke yao bila mafanikio.
Ushirikiano huu unatarajiwa kupunguza mzigo wa maandalizi na fedha kwa wenyeji katika mashindano makubwa kama haya, wakati huohuo ikionesha uwezo wa ushirikiano wa Uturuki na Jumuiya ya Ulaya katika michezo.
Na wakati UEFA ikianza kazi kwenye ofisi zao mpya za Istanbul, hotuba ya Erdogan inaashiria mipango mikubwa ya Uturuki kutambuliwa siyo tu kama kitovu muhimu cha michezo katika kanda, lakini sehemu muhimu duniani yenye uwezo wa kuandaa matamasha makubwa ya michezo.
Comments
No comments Yet
Comment