Dollar

38,1586

0.08 %

Euro

43,7541

0 %

Gram Gold

4.069,3400

-0.72 %

Quarter Gold

6.731,9300

0 %

Silver

39,7600

-1.06 %

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa hali inaweza kuzidi kuwa mbaya, hususani wakati ambapo serikali ya Marekani imesitisha kutoa misaada ya kibinadamu.

Machafuko DRC: Zaidi ya wakimbizi 40,000 wakimbilia Uganda

Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya wakimbizi 40,000 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchini Uganda wakikwepa machafuko katika eneo la mashariki la nchi hiyo.

Umoja huo, pia umesisitiza kuwa hali ya kibinadamu inaweza kuzidi kuwa mbaya, hususani wakati ambapo serikali ya Marekani imesitisha kutoa misaada ya kibinadamu.

Uganda imepakana na eneo la mashariki la DRC, ambalo linakumbwa na machafuko yaliyotokea baada ya waasi wa M23 kudhibiti baadhi ya maeneo.

Raia wengi wa DRC wamekimbia machafuko hayo, ambayo, kulingana na Umoja wa Mataifa yameua watu wapatao 900.

"Toka kuanza kwa mwaka, zaidi ya wakongomani 41,000 wamekimbilia Uganda kwa ajili ya usalama wao, huku idadi ya wakimbizi wa DRC waliopo Uganda ikifikia 600,000," alisema mwakilishi wa UNHCR nchini Uganda, Matthew Crentsil katika taarifa yake.

Tangu aingie madarakani, Rais Donald Trump wa Marekani umesitisha kutoa misaada ya kibinadamu kupitia shirika lake la USAID.

Hapo awali, shirika hilo lilikuwa limetenga bajeti ya dola bilioni 42.8, ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 42 ya misaada yote ulimwenguni.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#