Dollar

38,1588

0.3 %

Euro

43,6101

1.61 %

Gram Gold

3.958,7400

2.25 %

Quarter Gold

6.529,2600

2.67 %

Silver

39,4700

3.6 %

Raia wa Marekani, waliorejeshwa kutoka DRC wiki hii, wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama ya kutumia silaha za maangamizi na kushambulia kwa bomu majengo ya serikali na njama ya kuua na kuteka watu katika nchi ya kigeni.

Marekani yawashtaki waliohusika katika njama ya mapinduzi DRC

Wizara ya Sheria ya Marekani imewashtaki raia wanne wa nchi hiyo kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya watatu wao kurejeshwa Marekani juma hili, hii ni kulingana na kesi ya jinai iliyofunguliwa siku ya Jumatano.

Marcel Malanga, Tyler Thompson na Benjamin Zalman-Polun walipatikana na hatia nchini DRC ya kuhusika katika mapinduzi yaliyotibuka ya Mei 2024, ambapo watu waliokuwa na silaha walivamia nyumba za viongozi wakuu wa serikali na kudhibiti ofisi ya rais kwa muda katika mji mkuu Kinshasa.

Waliachiliwa huru siku ya Jumanne katika makubaliano yaliyokamilishwa baada ya mshauri mwandamizi wa masuala ya Afrika wa Rais Donald Trump, Massad Boulus kufanya ziara nchini humo.

Mtu wa nne, Joseph Peter Moesser, 67, anayedaiwa kutengeneza bomu, alikamatwa katika jimbo la Utah, nchini Marekani, Wizara ya Sheria ilisema katika taarifa yake.

Wanne hao wanakabiliwa na mashtaka ikiwemo njama ya kutumia silaha za maangamizi na kutaka kushambulia kwa bomu majengo ya serikali pamoja na njama ya kuwaua na kuwateka watu katika nchi ya kigeni, taarifa hiyo ilisema.

Makubaliano ya madini na DRC

"Washtakiwa walipanga, wakafanya utafiti, na kutambua watu watakaowalenga katika mapinduzi hayo, wakiwa na lengo la kuua watu, ikiwemo maafisa waandamizi wa serikali ya DRC," taarifa ilisema. "Waliwasajili wengine wajiunge katika njama hiyo kama wapiganaji wa jeshi la waasi na, wakati mwingine, waliwalipa watu kujiunga nao."

Malanga, Thompson na Zalman-Polun walikuwa miongoni mwa watu 37 waliopatikana na hatia ya kupanga njama ya makosa ya jinai, ugaidi na makosa mengine katika mahakama ya kijeshi ya Congo mwezi Septemba na kuhukumiwa kifo kutokana na jaribio hilo la mapinduzi.

Makubaliano kuhusu watu hao watatu walioachiliwa yanakuja wakati Marekani ikijadiliana na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, kuhusu uwezekano wa uwekezaji katika sekta ya madini.

Wanaume hao watatu wamekanusha kuhusika na uhalifu huo na wakajaribu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo bila mafanikio, kabla Tshisekedi wiki iliyopita kubadilisha hukumu ya kifo na kuwapa kifungo cha maisha jela, na baadaye kuwakabidhi wafungwa hao kwa mamlaka za Marekani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#