Sport
Dollar
38,1814
0.54 %Euro
43,6785
0.46 %Gram Gold
4.085,0600
0.53 %Quarter Gold
6.772,5700
0.78 %Silver
40,0000
0.58 %Mohamed Salah amekuwa katika hali nzuri msimu huu, kuelekea kuisaidia klabu hiyo kupata taji lake la 20
Mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah ameongeza mkataba wake wa kuwepo Anfield ambapo amekuwa kwenye timu hiyo kwa miaka minane, klabu hiyo ilisema siku ya Ijumaa.
"Bila shaka nimefurahi sana. Tuna timu nzuri kwa sasa. Kabla ya hapo, pia tulikuwa na timu nzuri. Lakini nimesaini mkataba kwa sababu nadhani tuna nafasi ya kushinda mataji mengine na kufurahia kucheza soka," Salah alisema katika taarifa.
"Ni jambo zuri sana; Nimefurahia kuwepo hapa. Nimecheza miaka minane; natarajia itakuwa 10. Nafurahia sana, nafurahia mchezo wangu. Nimekuwa na wakati mzuri katika klabu hii.

"Ningependa kuwaambia mashabiki kuwa, nimefurahi sana, tena sana kuwa hapa. Nimetia saini mkataba kwa sababu naamini kwa pamoja tunaweza kushinda mataji mengi. Endeleeni kutuunga mkono, na tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu, na natarajia baadaye tutaweza kushinda mataji mengi zaidi."
Wachanganuzi wanakiri kuwa ni jambo la kutia moyo kwa Liverpool kwa kuwa Salah amekuwa katika hali nzuri msimu huu, kuelekea kuisaidia klabu hiyo kupata taji lake la 20.
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Misri amefunga magoli 27 na amesaidia kupatikana kwa magoli 17 katika Ligi Kuu ya England msimu huu.
Akiwa na Liverpool, Salah ameshinda Ligi Kuu ya England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na makombe mawili ya Ligi pamoja na kombe la UEFA la Super Cup na lile la dunia la FIFA kwa vilabu.
Comments
No comments Yet
Comment