Sport
Dollar
38,0722
-0.16 %Euro
43,6342
-0.37 %Gram Gold
4.035,6500
-1.54 %Quarter Gold
6.720,2300
-0.17 %Silver
39,5500
-1.56 %Gachagua alipoteza baadhi ya ulinzi wake baada ya kuondolewa madarakani kama Naibu rais wa nchi hiyo kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa Oktoba 8, 2024.
Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amemuandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, Douglas Kanja akilalamikia usalama wa maisha yake.
Katika barua hiyo ya Aprili 15, 2025, Gachagua anadai kuwa kuna watu wanakula njama za kumdhuru.
Gachagua alipoteza baadhi ya walinzi wake baada ya kuondolewa madarakani kama Naibu rais wa nchi hiyo kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa Oktoba 8, 2024.
Katika barua hiyo, Gachagua ameainisha matukio kumi, ambayo anadai yanamlenga yeye na wafuasi wake.
Katika siku za karibuni, msafara wa Gachagua ulivamiwa na makundi yanayodaiwa kuwa ni ya vijana wahuni, ambao pia walifanya uharibifu mkubwa wa mali.
Gachagua alitolea mifano ya matukio ya Limuru, Nyandarua, Nyeri, Naivasha na Nairobi katika barua yake kwa IGP Kanja.
Hali kadhalika, toka aondolewe madarakani, Gachagua amekuwa mstari wa mbele kufichua matendo ya kifisadi yanayofanywa na serikali ya Rais William Ruto.
Katika moja ya mahojiano yake na vyombo vya habari, Gachagua aliwahusisha baadhi ya viongozi wa juu wa serikalini na biashara haramu ya dhahabu kutoka Sudan.
Pia, aliweka wazi ubadhirifu wa fedha za serikali kupitia miradi hewa, huku akihoji mahali zilipo fedha za miradi hiyo.
Katika barua yake kwa IGP wa Kenya, Gachagua ametaka kurudishiwa ulinzi wake binafsi na ule wa familia yake mara moja, kuacha kuandamwa na maafisa wa upelelezi na kuacha kuhujumiwa kwenye mikutano yake ya hadhara.
Pia amemuonya IGP kuwa atawajibika na lolote litakalomtokea.
Comments
No comments Yet
Comment