Dollar

38,2552

0.34 %

Euro

43,8333

0.15 %

Gram Gold

4.076,2000

0.31 %

Quarter Gold

6.772,5700

0.78 %

Silver

39,9100

0.36 %

Massad Boulos amesisitiza msimamo wa Marekani wa kuitaka ‘Rwanda kusitisha kuunga mkono kijeshi kundi la M23, na kuondoa vikosi vyake kutoka DRC'

Rwanda isitishe kuwaunga mkono kijeshi M23 - Mshauri wa Trump masuala ya Afrika

Massad Boulos, Mshauri mwandamizi wa masuala ya Afrika wa Rais Donald Trump amesisitiza msimamo wa Marekani kuwa “Rwanda iache kusaidia kijeshi kundi la M23 na iondoe vikosi vyake kutoka ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”

DRC na baadhi ya mataifa ya Magharibi ikiwemo Umoja wa Ulaya na Marekani wanashtumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23. Hata hivyo, Rwanda, inakanusha madai hayo.

Akihutubia waandishi wa habari kwa njia ya mtandao kufuatia ziara yake nchini DRC, Rwanda, Uganda, na Kenya, Boulos anasema pia alijadiliana na Rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu wapiganaji wa FDLR, kundi lenye silaha lililoko DRC ambalo linalaumiwa kwa mauaji ya kimbari ya 1994.

Ametaja hatari ya FDLR kuwa “kiungo muhimu” kwa makubaliano yoyote ya amani, Boulos amesema: “Kila mtu anatakiwa awe hana shaka na masharti ya makubaliano hayo, na wanatakiwa kujihisi salama kutokana na vitisho hivyo, iwe ni vya kweli au kuhofia uwezekano wa kutokea kwa vitisho baadaye.”

Tangu mwezi Januari, eneo la mashariki mwa Congo limekumbwa na matatizo ya usalama na hali mbaya kwa watu kufuatia mashambulizi mengine ya kundi la waasi la M23. Waasi hao wamedhibiti sehemu kubwa ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Mwezi Machi, Rais wa DRC Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano baada ya mazungumzo yaliyowashangaza wengi ambayo mpatanishi wake alikuwa kiongozi wa Qatar mjini Doha.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko mbioni kufikia makubaliano na Marekani ili ipate kuungwa mkono dhidi ya makundi ya waasi na Marekani ifaidike na madini yaliyoko kwenye taifa hilo.

Boulos aliongeza kuwa wakati wa ziara mjini Kinshasa, alizungumzia kuhusu mikataba ya madini na “kujadili muelekeo” wake na Rais Tshisekedi.

Alisema kuimarisha uwekezaji wa sekta binafsi ya Marekani nchini Congo, hasa katika uchimbaji madini, ni lengo ambalo wote wanakubaliana katika kuendeleza mafanikio ya nchi zote mbili.

“Bila shaka, tunahitaji kuwepo kwa mazingira ya utulivu ili tuweze kufanikisha lengo hili,” Boulos alisema.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#