Dollar

38,0754

-0.15 %

Euro

43,6584

-0.28 %

Gram Gold

4.028,3900

-1.72 %

Quarter Gold

6.720,2300

-0.17 %

Silver

39,4600

-1.81 %

Serikali ya nchi hiyo imeitaka mamlaka ya uwanja wa ndege wa Juba kumruhusu Makula Kintu, kuingia nchi hiyo, imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.

Sudan Kusini yamruhusu raia DRC kuingia nchini humo

Serikali ya Sudan Kusini imekubali kumpokea raia wa DRC aliyekuwa amefukuzwa nchini Marekani.

“Kama ishara ya uhusiano mzuri kati ya Sudan Kusini na Marekani, serikali yetu imekubali kumpa Makula Kintu kibali cha kuingia nchini mwetu,” alisema msemaji wa nchi hiyo Apuk Ayuel Mayen.

Kulingana na Mayen, mamlaka za uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba, zilitakiwa zimruhusu Kintu kuingia nchi hiyo ifikapo siku ya Jumatano.

Msemaji huyo ameongeza kuwa Sudan Kusini ipo tayari kufanikisha urejeshwaji wa raia wa Sudan Kusini wanaorudishwa kutoka nchini Marekani.

Siku ya Jumatatu, Wizara ya Mambo Nje ya Sudan Kusini, ilitangaza kuwasili kwa mtu aitwaye Nimeri Garang ambaye alizuiwa kuingia nchini humo, kabla ya kuja kubainika kuwa anaitwa Makula Kintu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#