Sport
Dollar
38,2552
0.34 %Euro
43,8333
0.15 %Gram Gold
4.076,2000
0.31 %Quarter Gold
6.772,5700
0.78 %Silver
39,9100
0.36 %'Ni wazi kuwa majadiliano hayajapewa nafasi kutokana na maamuzi yasiyo na msingi,' anasema waziri wa mambo ya nje
Siku ya Jumatano waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema uamuzi wa Algeria wa kuwatimua maafisa 12 wa Ufaransa "haufai" na "hauna msingi," huku hali ya wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili ikiongezeka.
"Tuko katika hali ambayo ni mbaya sana," Barrot amesema katika mahojiano na shirika la habari la Ufaransa la Inter, akionya kuwa hatua hiyo imesababisha majadiliano kati ya Ufaransa na Algeria kudorora zaidi.
"Kwa hakika ni suala la kudorora kwa mazungumzo kutokana na maamuzi yasiyo na msingi," alisema.
Alithibitisha kuwa Ufaransa imejibu kwa kuwafukuza maafisa 12 wa Algeria nchini humo pamoja na kumrejesha nyumbani balozi wao kutoka Algeria kwa ajili ya mashauriano.
"Tunaonesha, bila kusitasita, uwezo wetu wa kujibu inavyotakiwa na kwa njia thabiti," Barrot alisema.
Barrot alisisitiza kuwa Ufaransa haina nia ya kufanya hali kuzorota zaidi.
"Siamini kuwa tunahitaji kutunishiana misuli zaidi," alisema, akieleza kuwa Ufaransa inalenga kuendeleza dilplomasia.
Siku ya Jumatatu Algeria iliagiza maafisa 12 wa ubalozi wa Ufaransa kuondoka nchini ndani ya saa 48, baada ya kushtakiwa kwa wanaume watatu jijini Paris, mmoja wao akiwa mfanyakazi wa ubalozi wa Algeria nchini Ufaransa, kwa madai ya kuhusika na ugaidi.
Wakati Barrot akijizuia kuzungumzia mustakabali wa majadiliano wa nchi zote mbili, amesisitiza umuhimu wa kuanzisha tena mazungumzo.
"Siwezi kuzungumzia chochote kuhusu mustakabali wa mazungumzo yetu na Algeria kwa sasa," alisema.
"Nitasema hivi: Kama tunataka matokeo kwa raia wa Ufaransa, wakati huu au baadaye, lazima turejee katika majadiliano ya wazi, yenye malengo na mtazamo sahihi. Huo ndiyo msimamo wetu."
Comments
No comments Yet
Comment