Dollar

38,2552

0.34 %

Euro

43,8333

0.15 %

Gram Gold

4.076,2000

0.31 %

Quarter Gold

6.772,5700

0.78 %

Silver

39,9100

0.36 %

Erdogan ameendelea kukosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa kutumia kauli yake maarufu, ya “Dunia ni zaidi ya nchi tano,” akiwazungumzia wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo.

Uturuki ina ndoto ya kuwa na kanda yenye usuluhishi na sio migogoro— Erdogan

Pia, alisisitizia nafasi ya Ankara katika suala la usalama katika bara la Ulaya.Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametoa wito wa kuwepo haki kimataifa, maridhiano ya kikanda katika hotuba iliyotilia mkazo nafasi ya kidiplomasia ya Uturuki na ukosoaji wake dhidi ya mataifa ya magharibi kwa kushindwa kutatua majanga ya kibinadamu.

Akizungumza kwenye jukwaa la 4 la Kidiplomasia la Antalya lililofanyika siku ya Ijumaa, Erdogan alisisitiza umuhimu wa kuwa majadiliano katika utatuzi wa migogoro.

“Kwa mara nyingine tena, tunasisitiza kuwa tungependa kuona majadiliano wakati wa utatuzi wa migogoro,” alisema Erdogan katika risala yake mbele ya viongozi mbalimbali ulimwenguni, wanadiplomasia na wataalamu wa sera, kwenye jukwaa hilo lililoongozwa na kauli mbiu “Kuhuisha Diplomasia katika Dunia Iliyochangamana.”

Erdogan alirudia kulikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia kauli yake maarufu, “Dunia ni zaidi ya nchi tano,” akizungumzia wanachama wa tano wa kudumu wa baraza hilo.

“Kwa kuwa utu ni zaidi ya mataifa hayo,” alisema huku akisisitiza kuwa mfumo wa sasa wa utawala ulimwenguni hauakisi matarajio ya sasa.

Kwa muda mrefu sasa, Ankara imekuwa ikisisitiza mfumo ulio sawa unaotoa sauti kwa mataifa yanayoendelea.

Ujumbe wake kwa kanda: Uturuki bado ipo sana

Rais huyo wa Uturuki aliweka bayana kuwa Uturuki itaendelea kujiimarisha katika kanda, kupitia uhusiano wake wa karne na utambulisho wake kitaifa

“Sisi sio wakazi tu wa eneo hili, bali wamiliki halali,” alisema. “Tumekuwepo hapa kwa miaka 1000, na Mungu akipenda, tutaendelea kuwepo hapa kwa karne nyingi zijazo.”

Kauli ya Erdogan inakuja wakati Uturuki ikiboresha sera yake ya nje— ikiongeza nguvu kwenye nguvu yake kiuchumi na kuboresha mtandao wake kidiplomasia Kusini mwa Caucasus, eneo la Balkani na Mashariki ya Kati.

Uhuhishwaji wa uhusiano wa kimkakati na Marekani

Erdogan pia aligusia ushirikiano unaokuja na Marekani, ili kukuza biashara.

“Ni imani yangu kuwa katika muhula wa pili wa Rais Trump, kupitia mchango wa urafiki wetu, tutazidi kustawi katika kila eneo,” alisema Erdogan.

Alionesha utayari wa Uturuki wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Washington, akiweka msisitizo kwenye lengo la dola bilioni 100 kibiashara.

“Tumeupa mkakati huu kipaumbele kwa kuwa Marekani ni mshirika wetu,” alisema.

Akizungumzia mgogoro unaoendelea kuhusu masuala ya ushuru na ulinzi wa maslahi binafsi, Erdogan aliweka wazi mwelekeo wa Uturuki.

“Tutaendelea kuweka jitihada katika kuongeza ushindani wa kibiashara ili suala la ushuru lisiwe kipingamizi; nina hakika kuwa Uturuki itashinda katika azma hii,” aliongeza.

Mahusiano na Umoja wa Ulaya

Erdogan alidokezea kuhusu ombi la Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya, akisisitizia maslahi yanayofanana.

“Ni muhimu kwa Uturuki kuwa na nafasi ndani ya Umoja wa Ulaya. Tuko tayari kusukuma mbele mchakato huu tukitegemea hatua madhubuti kutoka Umoja wa Ulaya,” alisema.

Pia, alisisitizia nafasi ya Ankara katika suala la usalama ndani ya bara la Ulaya.

“Kwa mara nyingine tena, ni wazi kuwa usalama wa Ulaya haujakamilika bila Uturuki, ambayo tayari kubeba jukumu hilo katika siku zijazo,” aliongeza Erdogan wakati akizungumzia nafasi ya Uturuki kama mwanachama wa NATO.

Majadiliano ya Syria

Erdogan alielezea maendeleo ya Syria, akizitaka pande zote kutochezea nafasi hiyo adimu ya kurejesha utulivu nchini humo.

“Kutokana na mapinduzi ya Disema 8, hatutokuwa tayari kuichezea nafasi hii,” alisema, akionesha utayari wa Uturuki katika upatikanaji wa amani.

Akisisitizia nafasi ya kidiplomasia, Erdogan alionya dhidi ya tafsiri potofu kuhusu Ankara.

 “Tusieleweke tofauti katika msimamo wetu wa kutatua migogoro kupitia majadiliano,” alisema.

Kulingana na Erdogan, Uturuki inaendelea kuratibu namna ya kuipa Syria umoja na utawala.

 “Katika hili, tumekubaliana kuwa tutaendelea kushirikiana pamoja na Trump na Putin,” aliongeza Erdogan.

Akosoa mashambulizi ya Israeli, na ukimya wa ulimwengu

Katika moja ya kauli zake nzito, Erdogan alikosoa mashambulizi yanayoendelea kufanywa katika eneo la Gaza, akionya dhidi ya ukimya wa jumuiya ya kimataifa.

“Kukaa kimya dhidi ya mauaji haya ni kama kushiriki uhalifu huo,” alisema, akilenga taasisi za kimataifa kwa kushindwa kumaliza mgogoro huo.

"Mpango wa kusitisha mapigano utaendelea kuhujimiwa madhali Israeli inaendelea na ugaidi wake huko Gaza,” alisema.

Mara kwa mara, Uturuki imepaza sauti dhidi ya matendo ya Israeli huko Gaza.

Maono ya amani na ustawi

Erdogan alibainisha msimamo wa kikanda wenye kuweka msisitizo kwenye amani, maendeleo na ustawi shirikishi.

“Tunataka kuwa na kanda yenye kuthamini majadiliano dhidi ya umwagaji damu, machozi na maumivu,” alieleza huku akionesha tumaini la mustakabali uliotulia.

Kulingana na Erdogan, sera ya mambo ya nje ya Uturuki inalenga kuwa na ulimwengu salama si kwa vizazi vya sasa tu, bali na vizazi vijavyo.

“Tunatamani tuwarithishe watoto wetu dunia ya aina hiyo,” alisema.

Kuongezeka kwa nafasi ya Uturuki kidiplomasia

Jukwaa la Antalya limekuwa nafasi ya Uturuki kuwaleta pamoja viongozi na wanadiplomasia mbalimbali ulimwenguni.

Jukwaa la mwaka huu linafanyika wakati wa uwepo wa migogoro mbalimbali, ukiwemo ule wa Ukraine na Mashariki ya Kati.

Hotuba ya Erdogan iliweka msisitizo kwenye haki, ushirikishwaji na amani katika ulimwengu wa siasa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#