Sport
Dollar
38,4672
0.03 %Euro
44,0346
0.08 %Gram Gold
4.127,8000
-0.11 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Hata hivyo kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa, hakuna msamaha kwa watuhumiwa wa hujuma ya uchumi wa nchi, ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya watoto wachanga, ugaidi, biashara ya dawa za kulevya na uhalifu wa mtandaoni.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 4,887 katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Miongoni mwa watakaofaidi katika msamaha huo ni wafungwa wanaokabiliwa na hali maalum, kama vile wanawake waliofungwa na watoto wachanga na wafungwa wanaoishi na ulemavu wa akili.
Katika taarifa iliyochapishwa na wizara ya mambo ya ndani, vigezo vingi vimeelezewa juu ya wengine watakaopata msamaha huu ikiwemo wafungwa ambao wametumikia gerezani kwa angalau miaka miwili kufikia Machi 2, 2025.
Hata hivyo taarifa hiyo imebainisha wazi kuwa baadhi ya wafungwa hawatopata msamaha huo ikiwemo wale wa makosa makubwa kama vile kuhujumu uchumi wa nchi, ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya watoto wachanga, ugaidi, biashara ya dawa za kulevya na uhalifu wa mtandaoni.
Pia wafungwa ambao hapo awali walipokea msamaha wa rais lakini baadaye wakakosea tena au kukiuka kanuni za magereza pia hawastahiki kwa rehema hiyo ya sasa.
Wafungwa hao 4,887 waliobahatika na rehema ya Rais wataachiliwa kwa awamu ambapo 42 kati yao wataachiwa mara moja, huku waliobaki 4,845 wataendelea kutumikia vifungo vilivyopunguzwa.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais kuwapa msamaha wafungwa gerezani ambapo hatua hii husaidia katika kupunguza msongamano wa wafungwa na kuwapa rehema wafungwa wa makosa madogo madogo.
Mwaka 2021, Rais Samia aliwaachilia zaidi ya wafungwa 1500 huku wengine zaidi ya 3500 wakipunguziwa vifungo vyao maradufu.
Mnamo Disemba ya mwaka 2024 Rais Samia vile vile aliwaondolea au kuwapunguzia vifungo zaidi ya wafungwa 1526 katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania.
Wafungwa walioachiliwa walitakiwa kutumia mafunzo waliyopata gerezani katika ujenzi wa taifa na pia kuheshimu sheria za kitaifa.
Comments
No comments Yet
Comment