Sport
Dollar
38,1495
0.05 %Euro
43,6569
-0.27 %Gram Gold
4.088,0900
-0.26 %Quarter Gold
6.731,9300
0 %Silver
39,9400
-0.6 %Kiongozi huyo, Tadesse Worede, alikuwa naibu wa rais wa kanda hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na kamanda wa zamani wa TPLF wakati wa vita vya 2020-2022.
Siku ya Jumanne Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amemteua Tadesse Worede kuwa kiongozi wa mpito wa eneo la kaskazini la Tigray, ambapo mgawanyiko ndani ya chama tawala umezuwa hofu ya kuzuka kwa vita tena kati ya Ethiopia na Eritrea.
Tadesse, ambaye amekuwa naibu rais wa utawala wa eneo hilo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, alikuwa kamanda mwandamizi katika kundi la wapiganaji la TPLF wakati wa vita dhidi ya serikali kuu ya Ethiopia 2020-2022, ambapo maelfu ya watu waliuawa na mamilioni wengine kulazimika kuhama makazi yao.
Vikosi vya Eritrea vilisaidia serikali ya Ethiopia wakati wa mapigano hayo, lakini uhusiano kati ya mahasimu hao wawili umedorora na kufikisha kikomo makubaliano yaliyotiwa saini Novemba 2022.
Wachanganuzi wanasema majirani wa Ethiopia, Eritrea hawakufurahia kutojumuishwa kwenye makubaliano hayo, yaliyoruhusu TPLF, ambayo bado ina uhasama nao, kuongoza Tigray.
Hatari ya vita katika kanda
Mwaka uliopita kundi la TPLF liligawanyika mara mbili, huku upande mmoja ukiongozwa na Debretsion Gebremichael akishtumu uongozi wa mpito wa Tigray - ambao awali ukisimamiwa na msemaji wa TPLF Getachew Reda, ambaye kwa sasa miaka yake miwili imefikia kikomo - kwa kutozingatia maslahi ya watu wa Tigray.
Kundi la Debretsion, ambalo lilichukuwa udhibiti wa mji wa Adigrat mwezi uliopita, limekanusha madai ya uongozi huo ya kushirikiana na Eritrea, na kuzua hofu ya kuwepo kwa vita vya kikanda.
Kulingana na kundi la kutetea haki za binadamu mwezi uliopita Eritrea ilitoa amri kwa wanajeshi kujiandaa kwa vita. Ethiopia ilipeleka wanajeshi katika mpaka wake na nchi hiyo, ingawa Abiy amepuuza taarifa kuhusu uwezekano wa vita.
Tadesse, ambaye wachanganuzi wanasema hajaegemea upande wowote katika mgawanyiko wa TPLF, amekubaliana kuhusu masuala manane muhimu ikiwemo kurejea kwa watu walioondolewa katika makazi yao kutokana na vita na kuwapokonya silaha wapiganaji, kulingana na barua iliyosambazwa na msemaji wa Abiy, Billene Seyoum.
"(Tadesse) anafahamu vizuri uwezo na udhaifu wa utawala uliokuwepo, na wengi wanaamini yuko katika nafasi nzuri ya kuiongoza Tigray katika kipindi hiki muhimu," Abiy aliandika katika mtandao wa X.
"Ni matumaini yangu kuwa (Tadesse) atatumia fursa hii ya kihistoria kuwasaidia watu wa Tigray kufikia malengo yao ya amani na ustawi," aliongeza.
Comments
No comments Yet
Comment