Sport
Dollar
38,0945
0.11 %Euro
43,0515
-0.47 %Gram Gold
3.956,2900
0.75 %Quarter Gold
6.511,6500
0.65 %Silver
39,6400
0.15 %Mcebisi Hubert Jonas ni mwanaharakati mkongwe na mtumishi wa umma wa muda mrefu katika siasa na maendeleo ya Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemteua naibu waziri wa zamani wa fedha Mcebisi Jonas kuwa mjumbe maalumu nchini Marekani.
Uteuzi wa Jonas unakuja wiki kadhaa baada ta kufukuzwa kwa aliyekuwa balozi Ebrahim Rasool kufwatia mzozo kati yake na serikali ya Rais Donald Trump.
"Kwa hiyo natangaza uteuzi wa Bwana Mcebisi Jonas kama mjumbe wangu maalum nchini Marekani, akiwa kama mwakilishi rasmi wa rais na serikali ya Afrika Kusini," Ramaphosa alisema katika taarifa.
Mcebisi Hubert Jonas ni mwanaharakati mkongwe na mtumishi wa umma wa muda mrefu katika siasa na maendeleo ya Afrika Kusini.
Jonas alikuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini kati ya Mei 2014 na Machi 2017.
“Katika wadhifa huu, Bwana Jonas amepewa jukumu la kuyapa kipaumbele masuala ya Afrika Kusini ya kidiplomasia, biashara na ushirikiano. Ataongoza majadiliano, kujenga ushirikiano na kufanya vikao na maafisa wa serikali ya Marekani na wakuu wa sekta binafsi ili kuendeleza maslahi ya taifa letu,” taarifa ya serikali ilisema.
Hubert Jonas pia anafahamika kwa nafasi yake muhimu ya kuweka mifumo ya vyama vya ANC na SACP baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi katika maeneo ya Cape Mashariki na kuchangia katika kuundwa kwa serikali mpya ya mkoa mwaka 1994.
“Kama Naibu Waziri wa Fedha wa zamani wa Afrika Kusini, Bwana Jonas anakuja na uzoefu mkubwa kwa nafasi yake hii mpya ya ubalozi…Uteuzi huu unaonesha utumishi wake katika sekta ya umma na nia ya kuendeleza maslahi ya taifa ya Afrika Kusini pamoja na ya kiuchumi,” Ramaphosa alisema.
Serikali inasema bado imedhamiria kuendeleza ushirikiano wa faida kwa wote na Marekani.
“Kwa miongo kadhaa, Afrika Kusini na Marekani imekuwa na uhusiano wa kihistoria na wa kimkakati.
“Kwa maslahi ya nchi yetu, kanda yetu na bara letu, nasisitiza msimamo wetu wa kuimarisha na kuendeleza uhusiano huu kwa miongo kadhaa ijayo kwa misingi ya kuheshimiana, kutambua uhuru wa nchi zetu na faida kwa watu wetu,” taarifa hiyo iliongeza.
Comments
No comments Yet
Comment