Sport
Dollar
38,1252
0.09 %Euro
43,4067
0.69 %Gram Gold
3.976,3300
0.53 %Quarter Gold
6.511,6500
0 %Silver
39,6200
0.07 %Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini Tanzania (NIDA) imesema kuwa itasitisha matumizi ya namba za vitambulisho 634,124 kuanzia tarehe 1 Mei kwa wale ambao hawatakuwa wamechukua vitambulisho hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NIDA James Wilbert Kaji amesema kuwa kati ya vitambulisho milioni 1.2 ambavyo viko tayari ni 30% tu ambavyo vimechukuliwa.
Kaji alisema licha ya kuondolewa kwa masharti na muda wa mwisho wa kuchukua vitambulisho hivyo, bado kuna watu wengi ambao hawajafika kuvichukua.
NIDA inasema imetekeleza wajibu wake wa kuwatumia ujumbe mfupi wa simu (sms) lakini bado kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajajitokeza kuvichukua.
‘‘Sasa nawajulisha rasmi kuwa kuanzia tarehe 1 Mei,2025 tunafunga matumizi ya namba zao, mpaka watakapojitokeza kuchukua vitambulisho hivyo’’, Kaji aliwaambia waandishi wa habari.
Aliongeza kuwa baadhi ya watu wana dhana kuwa kwa kufahamu namba inatosha kuendeleza shughuli zake bila kuwa na kitambulisho.
Kusitishwa kwa matumizi ya namba hiyo kutasisitiza ulazima wa kuwa na kitambulisho chenyewe katika shughuli za kila siku.
Matumizi ya namba ya kitambulisho yatakapositishwa itakuwa vigumu kupata baadhi ya huduma muhimu.
Comments
No comments Yet
Comment