Sport
Dollar
38,4390
0.03 %Euro
44,0274
0.43 %Gram Gold
4.137,0200
0.9 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika inasema orodha ya bidhaa zilizoondolewa ushuru haijumuishi viwanda vya nguo, ambazo ndizo zinauzwa kwa wingi na mataifa wanachama nchini Marekani
Siku ya Jumanne Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeeleza hofu yake kuhusu ushuru uliowekwa na Marekani kwa bidhaa zinazoagizwa, ikiwemo zile zinazotoka kwa wanachama wa jumuiya yao.
Ushuru mpya wa 10% uliowekewa bidhaa zote zinazopelekwa Marekani uliotangazwa Aprili 2 ulianza kutumika Aprili 5, huku ushuru wa “kulipiza” ukitarajiwa kuanza kutekelezwa siku ya Jumatano.
Ushuru huu mpya utaathiri sana mataifa ya SADC kwa njia tofauti, huku bidhaa kutoka Lesotho zikiwekewa ushuru wa 50%, na Madagascar ikiwekewa 47%.
“Pamoja na kuwa Marekani imetangaza bidhaa ambazo hazitajumuishwa kwenye ushuru huu, nguo siyo miongoni mwa bidhaa hizi, ambazo zinapelekwa kwa wingi nchini Marekani na mataifa ya SADC,” Jumuiya hiyo ilisema katika taarifa.
Karibu mataifa yote ya SADC kwa sasa yanafaidika na mpango wa kutotozwa ushuru kwa bidhaa zinazopelekwa Marekani chini ya mpango wa AGOA.
Hata hivyo, ushuru huu utafikisha kikomo mpango huo wa AGOA, ambao ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
SADC inafanya tathmini ya kina kuhusu athari za hali hii kwa sekta mbalimbali, ili kujadiliwa katika mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni, kulingana na taarifa.
“SADC inasisitiza kuwa itaendelea kuimarisha malengo ya makubaliano ya kibiashara kama yalivyoainishwa na Shirika la Kimataifa linaloratibu Biashara Duniani (WTO) na iko tayari kujadiliana na wadau wote katika suala hili,” taarifa ilisema.
Nchi za Afrika zimekuwa zikijibu ushuru huo kwa njia tofauti tangu Rais Donald Trump alipotangaza.
Wiki iliyopita, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, aliweka ujumbe kwenye mtandao wa X, akitangaza kuondoa ushuru kwa bidhaa zote kutoka Marekani ‘‘ili kuwezesha uagizaji wa bidhaa kwa ajili ya soko la Zimbabwe, wakati huo huo akifungua milango ya kupanua soko la nje kwa bidhaa za Zimbabwe” zinazopelekwa Marekani.
Zimbabwe, moja ya nchi ya SADC iliyowekewa vikwazo vya Marekani kutokana na kukiuka haki za binadamu, watatozwa ushuru wa 18% kwa bidhaa zao.
Comments
No comments Yet
Comment