Sport
Dollar
38,2747
0.03 %Euro
43,6976
-0.01 %Gram Gold
4.071,7600
-2.14 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Kenya kuhusu Kazi na Ustawi wa Jamii inaripoti kuwa takriban wafanyakazi 80,000 wa Kenya wako Saudi Arabia na 60,000 katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), wengi wao wakiwa wafanyakazi wa nyumbani
Kenya imetangaza kuwa itaiunda kitenmgo maalum ndani ya idara ya polisi, kitakachokabilian ana usafirishaji haramu wa binadamu.
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen alisema kuwa taifa hilo limefadhaishwa na vitendo vya Wakenya kukabiliwa na mateso kwa visingizio vya kutafuta ajira nje ya nchi.
Baadhi ya Wakenya wamekuwa wakilalamika kuhadaiwa na mawakala wanaowatafutia kazi. kisha kuwatumbukiza katika giza la utumwa na mateso mikononi mwa waajiri wao nje ya nchi.
"Kama Wizara, tumeimarisha vita dhidi ya tabia hii mbaya na tunatazamia kuanzisha kitengo maalum cha kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu,’’ alisema Waziri Murkomen. ‘‘ Hii itahakikisha utekelezwaji mkali wa kanuni za uhamiaji wa wafanyakazi ili watu binafsi kuwarubuni vijana wetu kwa ahadi za maisha bora ya baadaye nje ya nchi," aliongeza Murkomen.
Malalamiko ya unyanyasaji
Mahitaji ya wafanyikazi wenye ujuzi wa chini katika nchi za Ghuba yameona uajiri wa watu katika tasnia ya utoaji huduma, wafanyikazi wa nyumbani na wajenzi.
Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Kenya kuhusu Kazi na Ustawi wa Jamii inaripoti kuwa takriban wafanyakazi 80,000 wa Kenya wako Saudi Arabia na 60,000 katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), wengi wao wakiwa wafanyakazi wa nyumbani.
Mnamo 2022, Saudi Arabia ilikuwa chanzo cha tatu kwa ukubwa cha kutuma pesa kwa Kenya, ikionyesha mwelekeo unaokua wa uhamiaji wa Wakenya katika eneo la Ghuba.
Licha ya hayo, wafanyakazi wa nyumbani wa Kenya katika Mashariki ya Kati wanaripoti hali duni ya kazi. Hii ni pamoja na muda mrefu wa kufanya kazi wa hadi saa 60 kwa wiki dhidi ya kiwango cha chini cha saa 48 kwa wiki kinachoidhinishwa na shirika la kazi ILO, unyanyasaji, udhalilishaji wa kingono, unyanyasaji, mwitikio duni wa malalamiko, na mawasiliano yaliyopunguzwa.
Soko la ndani haliwezi kumudu
Bunge la Kenya kupitia Kamati ya Kazi na Ustawi wa Jamii lilitaja ukosefu wa sheria na kanuni zisizotosha za kulinda ustawi wa wahamiaji wa Kenya kuwa mojawapo ya sababu zinazo endeleza unyanyasaji huu.
Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ilipendekeza kupigwa marufuku kwa muda kwa kuajiri na kusafirisha wafanyakazi wa ndani hadi Saudi Arabia mwaka wa 2022.
Hata hivyo, Wizara ya Kazi ilikataa ushauri huo, ikisema kuwa soko la kazi la ndani halingeweza kuchukua wafanyakazi wote wapya.
Comments
No comments Yet
Comment