Dollar

38,2900

0.06 %

Euro

43,7744

-0.03 %

Gram Gold

4.161,6900

0.02 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mwanamke mmoja, na watoto wake 2 walifariki baada ya kuangukiwa na ukuta wakati wa mvua kubwa

Watu 3 wafariki, na wengine wengi kuondoka katika makazi yao kutokana na mafuriko Nairobi, Kenya

Mvua kubwa ilionyesha katika mji mkuu wa Nairobi siku ya Jumanne imesababisha vifo vya watu watatu na wengine wengi wakiwa hawana makazi, polisi walisema.

Mwanamke mmoja na watoto wake wawili walifariki katika mtaa wa Mathare Phase 4 baada ya ukuta kuwaangukia nyumbani kwao wakati wa mvua kubwa. Polisi wanasema wawili hao walikufa papo hapo huku mmoja akifariki wakati akipelekwa hospitali.

Familia zaidi ya 500 zimelazimika kuhama makazi yao katika mitaa ya mabanda, mamlaka zinasema.

Maafisa wa huduma za dharura wamewataka wakazi kuchukua tahadhari huku Idara ya Hali ya Hewa nchini Kenya ikionya kuwa mvua hizi zitaendelea hadi 28 Aprili.

Mkurugenzi wa idara hiyo Dkt. David Gikungu anasema mvua kubwa zinatarajiwa katika maeneo mbalimbali kote nchini.

Wakazi wamesambaza video na picha katika mitandao ya kijamii zikionesha nyumba na magari yakisombwa na mafuriko.

Watumiaji wengi wa mitandao wamelaumu serikali kwa kushindwa kuimarisha mifumo ya majitaka, wakiteta kuhusu kushindwa kutimiza ahadi walizotoa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#