Sport
Dollar
38,1588
0.3 %Euro
43,6101
1.61 %Gram Gold
3.958,7400
2.25 %Quarter Gold
6.529,2600
2.67 %Silver
39,4700
3.6 %Katika Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya 2025, Emine Erdogan amewataka wadau wa dunia kufufua utamaduni wa uvumilivu na kujenga dunia ya haki ambapo amani itashinda vita, akigusia nafasi ya elimu katika kubadilisha dunia.
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan katika hotuba yake katika Jukwaa la 4 la Kidiplomasia la Antalya (ADF2025), amewataka viongozi wa dunia kuleta amani na haki kwa kuunganisha nguvu ya diplomasia na nafasi ya elimu.
Akishiriki katika mjadala wenye mada “Kujenga Mustakbali katika Dunia iliyogawanyika: Nafasi ya Elimu Kuleta Mabadiliko,” Emine Erdogan ameitaja elimu kama safari ndefu na kifaa muhimu katika kurekebisha dunia iliyogawanyika.
Ametilia mkazo kwamba kauli mbiu ya Jukwaa la mwaka huu, “Kurejesha Diplomasia katika Ulimwengu uliogawanyika,” inalenga moja kwa moja umuhimu wa ushirikiano katika dunia inayokabiliwa na hali ya taharuki.
‘Watoto hawawezi kuwa sehemu ya vita au migogoro’
Mke wa Rais amesema kwamba elimu ni safari inayomfanya binadamu kufikia uwezo wake wa juu kabisa.
“Kinachotufikisha katika safari hii yetu ndefu ni zana za kutuwezesha tunapoanza safari. Tunakwama katikati ya njia, taarifa muhimu zinapokosekana katika ramani hivyo tunachelewa,” amesema.
“Lengo la elimu sahihi na yenye viwango vya juu ni kumuinua kila mmoja.”
Akizungumzia mamilioni ya watoto waliopo katika maeneo ya vita na kukosa haki zao za msingi, Erdogan ameonyesha kusitikishwa kwamba elimu imekuwa kitu cha kifahari katika maeneo mingi ya dunia.
“Nasema kwa masikitiko makubwa: katika dunia ambayo tunashindwa kuwapa watoto wetu hata haki ya kuishi, haki ya elimu itakuwa mbali katika orodha.”
Amesisitiza kwamba jumuia ya kimataifa lazima ikabiliane na uhalisia.
“Sharti tuikumbushe jamii kwamba watoto hawawezi kuwa sehemu ya vita au migogoro,” amesema. “Tusisahau: dunia ambayo watoto wanauliwa kwa mabomu wakiwa katika usingizi iko hatiani.”
Erdogan amehitimisha kwa kutoa wito wa kuwaza mustakbali wenye matumaini: “Ningependa kuona dunia ambayo haina mapigano zaidi, ambapo watoto hawahisi chochote bali furaha, na kubeba migongoni mwao, sio mizigo mizito bali mabegi ya shule.”
Comments
No comments Yet
Comment