Dollar

38,2618

0.12 %

Euro

43,7512

-0.76 %

Gram Gold

4.185,7500

-0.56 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Shirika hilo la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa limelazimika kusitisha msaada kwa wanawake na watoto 650,000 kutokana na ukosefu wa fedha

Shirika la WFP laonya kuhusu 'viwango vya kutisha' vya utapiamlo nchini Ethiopia

Hali ya utapiamlo nchini Ethiopia imefikia "viwango vya kutisha" huku kina mama wajawazito pamoja na watoto milioni 4.4 wakihitaji matibabu ya haraka, shirika la mpango wa chakula WFP lilionya siku ya Jumanne.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Mkurugenzi wa WFP nchini Ethiopia, Zlatan Milisic, alisema katika majimbo ya Somali, Oromia, Afar, na Tigray idadi ya watoto waliokonda sana imepita 15% ambayo huwa ni kiwango cha dharura.

"Ethiopia inakabiliana na mzozo baada ya mzozo," Milisic alisema. "Kinachotupa wasiwasi ni kuwa ukame, mapigano, na kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi kunazidisha hali ya hatari ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi kwa jamii."

Watu zaidi ya milioni 10 kote nchini hawana chakula cha kutosha, ikiwemo watu milioni 3 walioondoka katika makazi yao kutokana na mapigano na athari za tabianchi, alisema.

Kulingana na afisa huyo, licha ya WFP kufikia watu zaidi ya milioni 3 kwa msaada wa chakula mwanzoni mwa 2025 -- shirika hilo limelazimika kusitisha matibabu kwa kina mama na watoto 650,000 wenye utapiamlo kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha.

Shughuli za kuwasaidia wakimbizi 800,000, ikiwemo wa Sudan 100,000, pia ziko hatarini, huku akiba ya msaada wa chakula na fedha ikitarajiwa kumalizika kufikia mwisho wa mwezi wa Juni, alisema. Kwa ujumla, watu milioni 3.6 huenda wakakosa msaada wa WFP hadi pale fedha zaidi zitakapopatikana.

Shirika la WFP linatoa wito wa kupatikana kwa dola milioni 222 kusaidia hadi Septemba kuendeleza shughuli zake na kuimarisha mipango yake ya 2025 ya kufikia watu milioni 7.2.

"Tuna maafisa wetu, tuna utaratibu mzima, na uwezo," Milisic alisema. "Kile ambacho tunakosa ni raslimali za kukabiliana na hali ilivyo kwa sasa."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#