Dollar

38,2763

0 %

Euro

43,7906

-0.86 %

Gram Gold

4.157,7800

-1.23 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Maafisa wa kijasusi wamefanikiwa kutibua mawasiliano kati ya afisa mmoja wa jeshi na viongozi wa kigaidi kuhusu taarifa za pale vikosi vya Burkina Faso vilipo, amesema waziri wa usalama.

Jeshi la Burkina Faso linasema limetibua jaribio la shambulizi kwa rais

Burkina Faso ilithibitisha siku ya Jumatatu kuhusu jaribio hilo la shambulizi kwa ofisi ya rais.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa ikiongozwa na viongozi wa jeshi tangu Septemba 2022 kufuatia mapinduzi yaliyoongozwa na Kapteni Ibrahim Traore, ambaye amekuwa akilaumu nchi ya Côte d'Ivoire kwa kuwapa hifadhi wapinzani wake.

Waziri wa Usalama wa Burkina Faso Mahamadou Sana alisema kupitia televisheni kuwa, idara ya ujasusi ya nchi inasema ilifanikiwa kusikiliza mawasiliano, kati ya afisa mmoja wa jeshi la Burkina Faso akitoa taarifa za sehemu ilipo vikosi vya nchi.

“Magaidi walipewa taarifa muhimu sana za kukabiliana na wanajeshi wetu na raia,zenye lengo la kuanzisha uasi dhidi ya mamlaka,” Sana alisema.

Waziri huyo alisema “njama hiyo kubwa” iliendelezwa kwa shambulizi katika ofisi ya rais tarehe 16 Aprili na kundi la wanajeshi ambao ni “maadui wa taifa”.

‘Kuchochea machafuko’

Sana alizungumzia kuhusu “waliopanga njama” wako nje ya nchi na wanafanya shughuli zao katika taifa la Côte d'Ivoire.

“Njama hii inaendeshwa sasa hivi kutoka kwenye kituo chao kikuu mjini Abidjan, kwa lengo la kuchochea machafuko nchini Burkina Faso kabla mwezi Juni,” aliongeza.

Wiki iliyopita, maafisa kadhaa wa jeshi walikamatwa na kufutwa kazi, kukiwa na hofu ya kuwepo kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

Miungano mingine

Serikali zinazoongozwa kijeshi za Burkina Faso, Mali na Niger ziliunda muungano wa mataifa ya Sahel (AES) Septemba 2023 kupitia makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama baina ya nchi hizo tatu za Afrika Magharibi.

Muungano huo umechukua hatua madhubuti za kuchagua washirika wengine kimataifa, ikiwemo kujiondoa kutoka kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Shirika la Kimataifa la nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF).

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#