Dollar

38,1448

0.45 %

Euro

43,5526

0.19 %

Gram Gold

4.082,0100

0.46 %

Quarter Gold

6.720,2300

0 %

Silver

39,9700

0.5 %

“Kama Uturuki, hatuna lengo la kupigana na nchi yoyote Syria, sio Israel tu,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan.

Uturuki haitaki mgogoro na nchi yoyote Syria-Fidan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amesisitiza kwamba Uturuki haina lengo la kuingia katika mgogoro na nchi yoyote ndani ya Syria, ikiwemo Israeli.

Akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja kupitia runinga ya CNN Turk siku ya Jumatano, Fidan amegusia masuala muhimu na kujibu maswali.

“Kama Uturuki, hatuna nia ya kupigana na nchi yoyote ndani ya Syria, sio na Israeli tu,” amesema, huku akisisitiza kwamba Syria ni taifa huru.

“Haikubaki kwa Israeli kujaribu kuichokoza Syria kwa kutumia malengo yake ya upanuzi katika kanda,” amesema.

Fidan amerudia tena kusema kuwa Uturuki haitaki kuingia katika mgogoro na nchi yoyote katika kanda lakini ametahadharisha kwamba, Ankara haiwezi kukaa kimya iwapo Syria kwa mara nyengine inakabiliwa na machafuko ya ndani, au uchokozi ambao unaweza kuhatarisha ulinzi wa taifa la Uturuki.

“Hatuwezi kukaa tu na kuangalia,” amesema.

Fidan pia ameilaumu Israeli kwa kuharibu miundombinu ya kijeshi ya Syria kufuatia kuanguka kwa utawala wa Assad, na kusema Tel Aviv imekuja na mkakati wa kutaka kuiacha serikali mpya ya Syria na vikosi vya ulinzi “bila kitu” na inakeleza hilo hatua kwa hatua.

“Hatuvamii wazi wazi nchi isiyotuvamia. (Lakini) kama kuna eneo linakosa usalama katika nchi jirani ambalo linaweza kutuathiri na sisi, hatuwezi kusimama na kuangalia,” amesisitiza, na kuongeza kuwa katika hali kama hiyo, Uturuki inachukua hatua, hatua za kidiplomasia.  

Akijibu swali kuhusu safari ya Marekani ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Fidan amesema, “Marekani inahitaji, kumuwekea mipaka Netanyahu na kuweka mfumo.”

Mawasiliano ya kiufundi na Israeli

Akizungumzia tuhuma za kuwepo kwa mazungumzo ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja kati ya Uturuki na Israeli, Fidan amesema: “Tunapofanya baadhi ya operesheni nchini Syria, kuna haja ya kuwa na utaratibu wa kuondoa migogoro na Israeli, ambayo inarusha ndege katika eneo hilo, kama tunavyofanya pamoja na Marekani na Urusi.”

“Kuna mawasiliano ya kiufundi (na Israeli) kuepusha kutoelewana,” amesema, na kuongeza kuwa mawasiliano hayo ya kiufundi yanafanywa moja kwa moja panapokuwa na ulazima.

Akizungumzia kuhusu uhusiano wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Rais wa Marekani Donald Trump, Fidan amesema, “Bwana Trump anamuheshimu Rais wetu kama kiongozi na ana uhusiano mzuri nae.”

Akipoulizwa lini Erdogan na Trump watakutana, alisema viongozi wote wanataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Kuhusu mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, Fidan amesema wamejadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo haja ya kuzuia mashambulizi ya Israeli Syria.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#