Sport
Dollar
38,0969
0.12 %Euro
43,0357
-0.5 %Gram Gold
3.952,8700
0.67 %Quarter Gold
6.511,6500
0.65 %Silver
39,6300
0.14 %Kiwango cha biashara cha Uturuki kimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, na kukuwa kutoka dola bilioni 3.6 hadi dola bilioni 36.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Burhanettin Duran amesisitiza ukuaji wa diplomasia na uchumi wa Uturuki na Afrika katika Jukwaa la 4 la Kidiplomasia la Antalya, lililofanyika katika wilaya ya Berek.
Jukwaa hilo limeratibiwa chini ya mwamvuli wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, na kuleta pamoja zaidi ya washiriki 6,000 kutoka nchi 155, ikiwemo viongozi wa nchi, mawaziri, wanadiplomasia, wasomi, taasisi zisizo za kiserikali, na waandishi wa habari.
Akizungumza na Anadolu, ambae ndie mshirika rasmi wa mawasiliano, Duran amegusia umuhimu wa jukwaa hilo.
“Kwa heshima, jukwaa la kidiplomasia tuliloliratibu chini ya mwamvuli wa rais wetu (Erdogan) na kuongozwa na Waziri wetu wa Mambo ya Nje Hakan Fidan lina umuhimu huu: Limewapa sauti watu ambao wasingeonekana au kusikika katika majukwaa mbalimbali duniani,” amesema.
Zaidi ya mikutano 230 ya pembeni imefanyika katika tukio hilo la siku tatu, ambalo liligusia mambo makubwa ya dunia kama zile Gaza, Ukraine, uhusiano wa Marekani-China-Urusi, vita vya biashara, na ulinzi wa Ulaya.
Akiangazia Afrika ilivyowakilishwa, Duran amesema imewakilishwa na viongozi 82 wa ngazi ya juu wa Afrika.
“Washiriki 82 wa ngazi ya juu, Afrika kwa mara nyengine imekuwa na mchango mkubwa katika Jukwaa la mwaka huu la Kidiplomasia la Antalya,” amesema.
Duran amesisitiza sera ya Uturuki kwa Afrika ya ‘pande zote mbili kunufaika’ na heshima ya pande mbili.
“Uturuki ni mdau wa kuaminika Afrika. Tunapouliza, ‘Sababu kubwa ya hii ni ipi?’ ni kwa sababu tunajenga uhusiano wa usawa. Hatuji kama ukoloni wa zamani. Kwa hiyo, tunahusika katika jitihada zinazochangia kwa nchi za Afrika, na kwa sababu wanaona hili, wanaiamini Uturuki,” amesema Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.
Kiwango cha biashara za Uturuki Afrika kimeongezeka katika miaka ya hivi karibuni, na kukua kutoka dola bilioni 3.6 mpaka dola bilioni 36.
Duran amesifia ongezeko hilo kutokana na mtandao mpana wa taasisi za taifa, ikiwemo Shirika la Ndege la Uturuki, Taasisi ya Maarif, Wakala wa Uratibu na Ushirika wa Uturuki, na Taasisi ya Emre Yunus.
Mbali na ushikiriano wa kiuchumi, Duran amegusia mchango wa Uturuki katika ulinzi na utulivu wa Afrika kupitia ushirikiano katika sekta yake ya ulinzi na msaada katika kupambana na ugaidi.
Amegusia jitihada za Uturuki zinazoendelea za upatanishi, akigusia Tangazo la Ankara la 2024 lililosainiwa kati ya Somalia na Ethiopia, na muendelezo wa mazungumzo yanayofuatia.
Akiangazia malengo mapana ya jukwaa, Duran alimalizia kwa kusema:
“Ilikuwa ni muhimu sana kuweka jukwaa ambapo matatizo ya dunia yangejadiliwa kwa kina, na kuwezesha kila mmoja kuja pamoja na kukumbatia diplomasia-kuliko migogoro na vita.”
Nchi za magharibi, amesema, walifuatilia kwa karibu yanayojiri katika jukwaa hilo.
“Naamini ujumbe wote uliowagusa umewasilishwa na washiriki na kupokewa kama ipasavyo.”
Comments
No comments Yet
Comment