Sport
Dollar
38,2636
0.07 %Euro
44,0617
-0.12 %Gram Gold
1.161,9100
0.48 %Quarter Gold
6.947,4100
0 %Silver
40,2900
0.29 %Mawaziri wa mambo ya nje wa Algeria, Uturuki wenyeviti wenza waratibu mkutano wa tatu wa mipango kati ya Uturuki na Algeria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf amesema kuwa nchi yake inalenga kuongeza kiwango cha biashara kati yake na Uturuki hadi dola bilioni 10, kufuatia mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan.
Mawaziri hao walikuwa wenyeviti wenza wa mkutano wa tatu wa mipango kati ya Uturuki na Algeria, uliofanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers siku ya Jumatatu.
Wakati wa mkutano huo, Attaf alieleza mafanikio yaliyopatikana kwa ushirikiano wa Uturuki na Algeria katika mpango ulioagizwa na Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune pamoja na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Mwaka uliopita, alisema mataifa hayo mawili yalifanya biashara ya pamoja ya kiwango cha dola bilioni 6, ambacho hakikuwa kimewahi kufikiwa, na kwa kuzingatia maelekezo ya viongozi wa nchi hizo mbili, wanalenga kuimarisha kiwango hiki hadi dola bilioni 10.
Attaf amesisitiza umuhimu wa kukabiliana na changamoto wakiwa na nia ya kutimiza malengo yao ya kimkakati, akisema uchumi wa Algeria unaendelea kutoa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwemo nishati endelevu, dawa, na kuimarisha ushirikiano wa mataifa yote mawili.
Comments
No comments Yet
Comment