Dollar

38,2636

0.07 %

Euro

44,0617

-0.12 %

Gram Gold

1.161,9100

0.48 %

Quarter Gold

6.947,4100

0 %

Silver

40,2900

0.29 %

Wapiganaji wa RSF hawajuzungumzia chochote kuhusu tukio hilo

Raia wasiopungua 33 wameuawa kwenye mashambulizi ya RSF katika mji wa El-Fasher,jeshi linasema

Raia wasiopungua 33 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya makombora ya wapiganaji wa RSF katika mji wa El-Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan, jeshi lilisema siku ya Jumatatu.

Taarifa ya jeshi ilisema kuwa wapiganaji wa RSF wamekuwa wakishambulia kwa makombora tangu siku ya Jumapili asubuhi.

Wapiganaji wa RSF hawajuzungumzia chochote kuhusu tukio hilo

Mapema wiki hii, kundi hilo la wapiganaji lilidai kuchukua udhibiti wa kambi ya wakimbizi ya Zamzam huko El-Fasher baada ya kukabiliana na vikosi vya jeshi.

Raia wasiopungua 400 waliuawa na karibu wengine 400,000 kuondolewa katika makazi yao kutokana na mapigano, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Kumekuwepo na mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF katika eneo la El-Fasher tangu Mei 2024, licha ya jumuiya ya kimataifa kuonya kuhusu hatari ya kupigana katika mji huo, ambao ni kitovu cha shughuli za misaada kwa ajili ya majimbo yote matano ya Darfur.

Tangu Aprili 15, 2023, RSF imekuwa ikikabiliana na wanajeshi wa Sudan kwa lengo la kudhibiti nchi, jambo lililosababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwepo na moja ya hali mbaya kwa watu duniani.

Zaidi ya watu 20,000 wameuawa kufikia sasa, na wengine milioni 15 kuondolewa katika makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na seriikali za mitaa. Hata hivyo utafiti kutoka kwa wanazuoni wa Marekani, unakadiria kuwa waliouawa ni karibu 130,000.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#