Sport
Dollar
38,2489
0.07 %Euro
44,0461
-0.14 %Gram Gold
1.162,7000
0.42 %Quarter Gold
6.947,4100
0 %Silver
40,3000
0.32 %Rais Putin alieleza msimamo wake kuhusu umuhimu wa kuondosha chanzo cha vita hivyo na kuhakikisha maslahi ya usalama wa Urusi, serikali ya Urusi imesema.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kujadili ushirikiano na hali ilivyo nchini Ukraine, serikali ya Urusi ilisema Jumatatu.
Viongozi hao wawili walifanya tathmini ya uwezekano wa kuimarisha ushirikiano utakaofaidi pande zote mbili, hasa biashara, uchumi, na uwekezaji.
“Kwa kuzingatia maslahi ya Afrika Kusini katika kusaidia kupata suluhu ya amani katika mzozo wa Ukraine, Vladimir Putin ameeleza msimamo wa Urusi wenye lengo la kuondoa chanzo cha mgogoro na kuhakikisha maslahi ya usalama wa Urusi,” serikali ilisema.
Putin pia alimpongeza Ramaphosa na watu wa Afrika Kusini wakati wakijiandaa kusherehekea siku ya Uhuru, ambayo huadhimishwa tarehe 27 Aprili.
Marais hao wawili walikubaliana kuendelea kushirikiana katika ngazi mbalimbali.
Comments
No comments Yet
Comment