Dollar

38,4237

0.22 %

Euro

43,7574

-0.04 %

Gram Gold

4.055,2400

-1.8 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Barani Afrika WHO inasema tangu mwaka wa 2000, zaidi ya wagonjwa wa malaria bilioni 1.7 na vifo milioni 12 vimepukwa katika kanda ya Afrika kutokana na juhudi za kimataifa za afya.

Dunia yaadhimisha siku ya malaria, nchi 9 Afrika bila malaria

Huku dunia ikiadhimisha Siku ya Malaria Duniani, 25 Aprili 2025, Shirika la Afya Duniani (WHO) linatoa wito wa kuhuishwa juhudi katika ngazi zote, kuanzia sera ya kimataifa hadi hatua za jamii, ili kuharakisha maendeleo kuelekea kutokomeza malaria.

"Historia ya malaria inatufundisha somo gumu: tunapopotosha mawazo yetu, ugonjwa huongezeka, na kuathiri zaidi watu walio hatarini zaidi," Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, viongozi wa dunia waliweka msingi wa maendeleo katika udhibiti wa malaria duniani, ikiwa ni pamoja na kuzuia wagonjwa wa malaria zaidi ya bilioni 2 na takriban vifo milioni 13 tangu 2000.

Hali ilivyo Afrika

Afrika inasalia kuwa eneo lililoathiriwa zaidi, likichukua takriban 94% ya wagonjwa duniani na 95% ya vifo mwaka 2023.

Takwimu za WHO zinaonyesha maambukizi milioni 246 mwaka jana.

Zaidi ya nusu ya wagonjwa wote kimataifa walitokea katika nchi tano tu za Kiafrika, zikiwemo Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Ethiopia na Msumbiji.

Takriban wanawake wajawazito milioni 12.4 katika nchi 33 za Afrika zilizo katika hatari kubwa walipata malaria mwaka wa 2023. Hatua zinazolengwa zinatajwa kuzuia takriban kesi 551,000 za kuzaliwa kwa uzito mdogo.

Hadi sasa, WHO imeidhinisha nchi 45 na eneo 1 kuwa salama kutokana na malaria, na nchi nyingi zilizo na mzigo mdogo wa malaria zinaendelea na jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.

Kati ya hizi nchi 9 barani Afrika zimetokomeza au hazijawahi kuwa na malaria.

Kazi bado ni kubwa

Kati ya nchi 83 zilizosalia zenye ugonjwa wa malaria, 25 ziliripoti chini ya kesi 10 za ugonjwa huo mnamo 2023.

Walakini, kama historia inavyoonyesha, mafanikio haya ni dhaifu.

"Lakini historia hiyo hiyo pia inatuonyesha kile kinachowezekana: kwa dhamira thabiti ya kisiasa, uwekezaji endelevu, hatua za sekta mbalimbali na ushirikishwaji wa jamii, malaria inaweza kushindwa,” Adhanom ameongezea.

Barani Afrika WHO inasema tangu mwaka wa 2000, zaidi ya wagonjwa wa malaria bilioni 1.7 na vifo milioni 12 vimeepukwa katika kanda ya Afrika kutokana na juhudi za kimataifa za afya.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#