Sport
Dollar
38,4214
0.2 %Euro
43,7725
-0.03 %Gram Gold
4.064,3000
-1.58 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kamati huru itafanya ukaguzi wa kina wa huduma zote za upandikizaji wa figo katika hospitali ya Mediheal iliyopo kaunti ya Eldoret katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, baada ya hospitali hiyo kushutumiwa kwa kuhusika na mauzo ya figo.
Waziri wa Afya nchini Kenya imezindua Kamati Huru ya Uchunguzi kuhusu Huduma za Kupandikiza viungo. Kamati hiyo ina wataalamu 13.
Kamati hiyo, inayoongozwa na Prof. Elizabeth Bukusi, mwanasayansi mkuu mwandamizi wa utafiti wa kimatibabu katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (KEMRI).
Lengo lake ni kujibu hoja za wananchi juu ya tuhuma kubwa za ukiukwaji wa maadili na taratibu za upandikizaji wa viungo katika Hospitali ya Mediheal Group of Hospitals iliyoko kaunti ya Eldoret ambayo imejipata katika kashfa ya huduma isiyo halali.
Hii inafuatia malalamiko kutoka kwa Wakenya kadhaa kuwa figo zao zilitolewa katika hospitali ya Mediheal, katika kaunti ya Eldoret ilhali hawakulipwa fedha zote walizoahidiwa.
“Kufuatia wasiwasi wa hivi majuzi uliotolewa na Jumuiya ya Upandikizaji na madai yanayoibuka kuhusu huduma za upandikizaji katika Hospitali ya Mediheal Group, Wizara, kwa ajili ya usalama wa mgonjwa na uaminifu wa umma, imeanzisha hatua kadhaa muhimu,” Maru Muthoni , Katibu mluu wa huduma ya umma ya afya amesema.
"Huu ni wakati wa kuwajibika. Hatufanyi uchunguzi tu - tunarejesha imani ya umma katika mfumo wa afya,” Waziri wa Afya Adan Duale amesema.
“Hatutavumilia kuwa katika hali ya kutojali au kuficha makosa yoyote," alisema Duale huku akiitaka kamati hiyo kuzingatia uadilifu, uwazi, busara na weledi.
Waziri wa Huduma za Matibabu Dkt. Ouma Oluga aliitaka kamati hiyo kutekeleza kazi yake kwa ukamilifu na kuwasilisha ripoti ambayo itasaidia kurahisisha utendakazi wa kimatibabu katika vituo vyote vya afya nchini Kenya.
Akithibitisha kuunga mkono kikamilifu Wizara, Waziri Duale aliikumbusha kamati hiyo kutoa ripoti ya kina ifikapo tarehe 22 Julai 2025.
"Tutachukua hatua madhubuti, kwa uwazi, na kwa manufaa ya watu wa Kenya," aliongeza.
Baraza la Wanasheria la Kenya, LSK limeongezea sauti kwa kukashifu huduma ambayo imegunduliwa kuwa ya kuwadhulumu waliotolewa viungo vyao.
“LSK inaelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya ripoti za hivi majuzi za washukiwa wa ulanguzi wa viungo, haswa, figo, ndani ya vituo fulani vya afya nchini Kenya, huku Hospitali ya Mediheal, Eldoret, ikitajwa haswa kama mhusika mkuu katika madai haya,” rais wa LSK Faith Adhiambo alisema katika taarifa.
“Ni maoni yetu kwamba hali iliyopo si tu kwamba haikubaliki, bali inataka uingiliaji wa haraka na wadau tofauti wanaohusika kwa njia mbalimbali,” Adhiambo ameongezea.
Hospitali hiyo husika ya Mediheal Group of Hospitals imekanusha madai ya kuhusika na ulanguzi wa figo, na kuyataja madai hayo kuwa hayana msingi na uongo.
Hospitali hiyo inasema inatoa huduma ya upandikizaji wa figo na upasuaji mwingine wa hali ya juu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya maadili na taaluma.
Imekana kuhusika na mauzo ya viungo vya watu.
Kamati huru itafanya ukaguzi wa kina wa huduma zote za upandikizaji wa figo kwa hospitali ya Mediheal katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa kuzingatia utawala, mbinu za kimatibabu, kufuata maadili na viwango vya usalama vya wagonjwa.
Comments
No comments Yet
Comment