Dollar

38,4203

0.21 %

Euro

43,6184

-0.36 %

Gram Gold

4.059,6900

-1.69 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Haya yanajiri baada ya Wizara ya Elimu kutangaza kuwa masomo ya hesabu hayatakuwa ya lazima tena kwa wanafunzi wa sekondari chini ya Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC), mabadiliko makubwa kutoka kwa mfumo ulioondolewa wa elimu.

Kenya yaamua tena hisabati kuwa somo la lazima

Wizara Elimu ya Kenya imeamua kubatilisha uamuzi wake wa awali wa kufuta somo la hesabu katika ngazi ya shule ya upili.

Akizungumza wakati wa majadiliano ya Kitaifa kuhusu Mtaala Unaozingatia Umahiri (CBC) Alhamisi, Waziri wa Elimu Julius Migos alisema kuwa uamuzi huo ulifanywa baada ya wadau wengi wakati wa mijadala ya CBC kutaka somo la hisabati liwepo katika shule ya upili.

Hii ina maana kwamba wanafunzi ambao watachagua fani ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati) watasoma Hisabati ya hali ya juu na wanafunzi watakaochagua njia nyingine mbili watasoma Hisabati iliyorahisishwa.

"Aina fulani ya masomo ya hesabu itafanywa kuwa ya lazima kwa njia mbili, watakaofanya masomo ya sayansi STEM watahitajika kufanya hesabu ya ndani zaidi, lakini bado kutakuwa na hesabu ya kawaida kwa wale watakaofanya masomo mengine," alisema Waziri Migos, akiongeza kuwa mazungumzo zaidi yalifanyika na Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD).

Haya yanajiri baada ya Wizara ya Elimu kutangaza kuwa masomo ya hesabu hayatakuwa ya lazima tena kwa wanafunzi wa sekondari chini ya Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC), na hivyo kuashiria mabadiliko makubwa kutoka kwa mfumo ulioondolewa wa 8-4-4.

Wataalamu wamepinga vikali kuondoloewa kwa masomo ya hesabu.

"Hesabu ni somo muhimu kwa ajili ya kujenga nguvu kazi yenye uwezo kwa karne ya 21. Hakika, Hesabu pia ina matumizi mapana katika mafunzo ya maeneo mengine yote ikiwa ni pamoja na ubinadamu, michezo na bila shaka masomo ya sayansi ya STEM."

Katika mfumo huo mpya wa CBC wanafunzi watachukua masomo manne ya lazima, ambayo ni; Lugha ya Ishara ya Kiingereza ya Kenya au ya Kimataifa, Kiswahili, Elimu ya Kimwili, na Mafunzo ya Huduma kwa Jamii.

Kisha watachagua masomo mengine matatu kutoka kwa kundi la masomo 38.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#