Tokyo: 06:34 PM
Londra: 09:34 AM
New York: 04:34 AM
İstanbul: 12:34 PM

Dollar

38,1853

0.56 %

Euro

43,6059

0.31 %

Gram Gold

4.086,1900

0.56 %

Quarter Gold

6.756,6000

0.54 %

Silver

40,0100

0.6 %

Waziri wa Afya wa Kenya Aden Duale ametangaza kuwasili kwa chanjo 10,700 za Mpox kwa lengo la kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Kenya yapokea chanjo zaidi ya 10,000 kukabiliana na ugonjwa wa Mpox

Waziri Duale anasema chanjo hizo zimepatikana kutokana na ushirikiano wa serikali na mashirika mbalimbali ikiwemo shirika la kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC, shirika la afya duniani, WHO, UNICEF na GAVI.

“kuwasili kwa chanjo hizi ni hatua muhimu katika juhudi za serikali za kukabiliana na mlipuko na maambukizi ya Mpox katika jamii,” alisema.

Alisema chanjo ya Mpox itatumika kama hatua za ziada katika mpango mpana wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Wizara ya Afya imetoa wito kwa watu kuchukua tahadhari na kujilinda na Mpox kwa kuzingatia utaratibu wa kinga wa afya ya umma.

Hii ni pamoja na kuepuka kutangamana na watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya Mpox pamoja na kuepuka kutumia vitu vya pamoja, kutumia njia sahihi za usafi, kwa kunawa mikono kila wakati, na kupunguza kutangamana na mwenza wako.

Tangu kutangazwa kwa mlipuko huo 31 Julai, 2024, maambukizi 67 ya Mpox yamethibitishwa kote nchini Kenya.

Kulingana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mary Muthoni Muriuki, anasema kufikia sasa watu 49 wamepona, 1 amefariki na wengine 327 wanafwatiliwa kwa karibu kubaini zaidi kuhusu afya zao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#