Dollar

38,2618

0.12 %

Euro

43,7920

-0.66 %

Gram Gold

4.179,3100

-0.72 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Katika wosia wake, Papa Francis alieleza sehemu maalum anapotaka kuzikwa, pembeni pa basilica, hata kuongeza mchoro ulioambatanishwa kwa maelezo zaidi

Kwenye ardhi, bila mapambo: Papa Francis alitaka mazishi ya kawaida

Papa Francis alieleza mambo ambayo angetaka yafanyike akishafariki katika wosia wake, akiomba azikwe katika kaburi la kawaida lisilo na mapambo, ndani ya kanisa lake pendwa la Santa Maria Maggiore.

“Nikihisi kwamba maisha yangu duniani yanakaribia mwisho na nikiwa na matumaini makubwa ya Uzima wa Milele, ningependa kuacha wosia wangu kuhusu mahali ambapo nitazikwa,” aliandika papa katika wosia wake wa tarehe 29 Juni 2022, ambao ulisambazwa na Vatican siku ya Jumatatu.

“Ninaomba kwamba mwili wangu ulazwe kungoja siku ya ufufuo katika Basilica ya Santa Maria Maggiore,” aliandika papa, aliyekuwa na mazowea ya kutembelea kanisa hili muhimu la Katoliki kabla na baada ya safari zake zote kama papa.

Vatican imetenga eneo maalumu chini ya kanisa la Mtakatifu Petro ambamo wamezikwa mapapa 100. Papa Francis atakuwa papa wa kwanza katika kipindi cha miaka 100 kuzikwa nje ya Vatican.

Katika wosia wake, Francis alitaja sehemu maalum anapotaka kuzikwa, pembeni pa basilica, hata kuongeza mchoro ulioambatanishwa kwa maelezo zaidi, na akasema gharama za maziko zilipangwa awali.

“Kaburi lazima liwe kwenye ardhi, la kawaida, na bila mapambo maalum ila maandishi pekee: Franciscus.”

Katika mwisho wa wosia wake, kiongozi wa kiroho wa Wakatoliki duniani alimwomba Mungu “awabariki wale walionipenda na watakaoendelea kuniombea”.

“Nilijitolea kwa mateso niliyopitia siku za mwisho za maisha yangu kwa Mungu kwa ajili ya amani duniani na undugu kwa watu wote.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#