Dollar

38,1284

0.08 %

Euro

43,3327

0.61 %

Gram Gold

3.962,0300

0.17 %

Quarter Gold

6.511,6500

0 %

Silver

39,6000

0.02 %

Maafisa wa Palestina wamelaani hatua hiyo ikiwa ni mtindo unaoendelea na tayari zaidi ya walowezi 13,000 wamevamia Msikiti huo tangu kuanza kwa mwaka 2025.

Walowezi zaidi 1,200 wa Israeli wavamia Msikiti wa Al-Aqsa

Maelfu ya walowezi wa Israeli waliingia kwa nguvu katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa kwenye sehemu inayokaliwa ya Jerusalem Mashariki, ikiwa ni siku ya tatu ya sherehe ya Pasaka ya kiyahudi, afisa mmoja wa Palestina alisema.

Afisa huyo anayefanya kazi na Idara ya masuala ya Dini ya Palestina huko Jerusalem alisema Jumanne walowezi wa Israeli wasiopungua 1,220 waliingia kwenye eneo linalozozaniwa wakipewa ulinzi na polisi wa Israeli kuanzia asubuhi.

Walioshuhudia wanasema walowezi waliingia katika mlango wa Al-Mugharbah, upande wa magharibi wa msikiti.

Karibu walowezi 1,149 waliingia kwa nguvu kwenye eneo hilo siku ya Jumatatu na wengine 494 waliingia siku ya Jumapili kuadhimisha sherehe hizo za wiki nzima.

Kutoka

Pasaka ya Kiyahudi inaadhimishwa kukumbuka kipindi ambacho ‘Waisraeli’ walivyotoka Misri wakati wa Mtume Musa na inasherehekewa kama sikukuu muhimu ya kidini kwa Wayahudi.

Kulingana na Wizara ya Masuala ya kidini ya Palestina, walowezi walivamia msikiti huo mara 21 mwezi uliopita, wakati Waislamu wakiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Takwimu zilizotolewa na gavana wa Jerusalem zinaonesha walowezi wa Kiyahudi 13,064 walivamia msikiti huo robo ya kwanza ya mwaka 2025.

Tangu 2003, Israeli imeruhusu walowezi kuingia katika eneo hilo kila siku, isipokuwa siku za Ijumaa na Jumamosi pekee.

Msikiti wa Al-Aqsa ni sehemu ya tatu tukufu kwa Waislamu. Wayahudi wanauita "Mlima wa Hekalu," wakidai kuwa ilikuwa eneo la mahekalu mawili ya Kiyahudi siku za kale.

Israeli ilikalia Jerusalem Mashariki, ambapo kuna msikiti wa Al-Aqsa, wakati wa vita vya 1967 vya Waarabu na Waisraeli. Ikajichukulia mji mzima mwaka 1980 katika hatua ambayo haijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#