Dollar

38,0076

0.07 %

Euro

41,6557

-0.1 %

Gram Gold

3.698,9700

-0.31 %

Quarter Gold

6.191,9000

-1.24 %

Silver

36,8200

1.85 %

Mali inaituhumu Algeria kwa kudungua ndege yake ya ujasusi isiyo na rubani katika eneo la mpaka wiki iliyopita.

Mali, Burkina Faso, Niger zawaita mabalozi wake kutoka Algeria

Mali imeituhumu nchi jirani ya Algeria kwa kudungua moja ya ndege zake za ujasusi zisizo na rubani karibu na eneo la mpaka wa nchi hizo mbili, hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa siku ya Jumapili na Wizara ya Ulinzi kupitia runinga ya taifa.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi na washirika wake Burkina Faso na Niger zitawaita mabalozi wake kutoka Algeria kwa mashauriano kufuatia tukio hilo, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili.

Mali imesema, mabaki ya ndege hiyo yalipatikana umbali wa kilomita 9.5 kusini mwa mpaka na Algeria baada ya kudunguliwa usiku wa kati ya Machi 31 na Aprili 1.

‘kitengo cha kutowajibika’

Serikali imesema kwamba ina uhakika ndege ya jeshi la Mali iliharibiwa katika hatua ya kikatili iliyopangwa na utawala wa Algeria.”

Nchi hizo tatu za Sahel katika taarifa yake ya pamoja zimesema kwamba zinalaani “hatua hiyo ya serikali ya Algeria.”

Wizara ya Ulinzi ya Algeria Aprili 1 imesema jeshi limedungua “ndege isiyo na rubani ya ujasusi” ambayo ilikiuka anga ya nchi ya Afrika Kaskazini karibu na Tinzaouaten, liililopo karibu na mpaka, bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Jeshi la Mali limesema katika taarifa yake wakati huo kwamba moja ya ndege zake zisizo na rubani ilianguka ilipokuwa katika shughuli za kijajusi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#