Tokyo: 02:23 AM
Londra: 05:23 PM
New York: 12:23 PM
İstanbul: 08:23 PM

Dollar

38,1588

0.3 %

Euro

43,6101

1.61 %

Gram Gold

3.958,7400

2.25 %

Quarter Gold

6.529,2600

2.67 %

Silver

39,4700

3.6 %

Maafisa watano wa Kenya waliripotiwa kutekwa nyara na kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Maafisa wa Kenya waliotekwa nyara waachiliwa huru baada ya miezi miwili

Maafisa watano wa Kenya wameachiliwa huru, Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen alisema Jumatatu, miezi miwili baada ya kutekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini mashariki mwa nchi.

Watu wenye silaha wanaoaminika kuwa wa kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mafungamano na al Qaeda waliripotiwa kuwateka nyara machifu wa vijiji, ambao walikuwa maafisa wa eneo , katika kaunti ya Mandera mwezi Februari karibu na mpaka wa Somalia, ambako kundi hilo lina makao yake.

"Tuliamua kufanya kazi pamoja na jamii, na kufanya kazi na serikali ya kaunti ya Mandera, na mchakato huu umezaa matunda," Murkomen aliwaambia wanahabari, kulingana na kanda ya televisheni ya NTV Kenya iliyoonekana kwenye mtandao wa X.

Murkomen alisema machifu hao sasa wako mikononi mwa mamlaka ya Kenya na kwamba "watawasili nyumbani hivi karibuni," ingawa hakusema kama al-Shabaab walihusika na utekaji nyara huo.

Hata hivyo, wakati wa tukio, wasimamizi wa eneo hilo walikuwa wameshuku kuwa magaidi wa al-Shabaab ndio waliohusika na utekaji nyara huo.

Kundi hilo hadi sasa halijasema lolote kuhusu utekaji nyara huo. Al Shabaab imekuwa ikipigana kwa miaka mingi nchini Somalia na mara kwa mara hufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka nchini Kenya.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#