Dollar

38,1216

0.08 %

Euro

43,5819

1.01 %

Gram Gold

4.006,7100

1.3 %

Quarter Gold

6.511,6500

0 %

Silver

39,6300

0.09 %

Haya yanatokea siku kadhaa baada ya Algeria kuwapa maafisa 12 wa Ufaransa saa 48 kuondoka nchini humo.

Ufaransa yamrejesha nyumbani balozi wake wa Algeria huku wasiwasi ukiongezeka

Siku ya Jumanne Ufaransa imesema imewafukuza maafisa 12 wa Algeria, huku kukiwa na hali ya kutoelewana kati ya mataifa hayo mawili baada ya maafisa 12 wa Ufaransa kutimuliwa Algiers.

Hatua hii inatokana na uamuzi wa Algeria siku ya Jumatatu wa kuwataka maafisa wa ubalozi wa Ufaransa kuondoka nchini mwao ndani ya muda wa saa 48, baada ya tuhuma za kuhusika na uhalifu wa ugaidi dhidi ya wanaume watatu jijini Paris, ambapo mmoja wao ni afisa wa ubalozi wa Algeria nchini Ufaransa.

“Kama njia ya kujibu maamuzi yao yasiyo ya msingi na yasiyoeleweka, tunawatimua maafisa wa Algeria 12 na kumrejesha nyumbani balozi wetu kwa ajili ya mashauriano,” Waziri wa Mambo ya Nje Jean Noel-Barrot aliandika katika mtandao wa X.

Alisema anajibu “kama ilivyotangazwa” tangu Algeria kuchukua hatua ya “kuleta taharuki.”

“Tuko tayari kwa mazungumzo wakati wowote, lakini siyo kuegemea upande mmoja,” aliongeza.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Ufaransa ya taifa dhidi ya uhalifu wa ugaidi imethibitisha kuwa washukiwa hao walishtakiwa kwa makosa ya kukamata watu, utekaji, kuzuia watu kinyume cha sheria na kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi.

Awali Barrot aliitaja hatua hiyo ya Algeria "kuwa mbaya" na kuonya kuwa "itawaletea matatizo."

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#