Dollar

38,2844

0.04 %

Euro

43,3690

-0.8 %

Gram Gold

4.087,9900

-1.75 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipelekwa hospitali kabla ya mechi na mchezo ukasimamisha baada ya kipindi cha kwanza walipopewa taarifa kuwa amefariki.

Mchezaji wa soka Afrika Kusini afariki kabla ya mechi yao ya ligi

Mchezaji wa Afrika Kusini Sinamandla Zondi amefariki siku ya Jumanne baada ya kuanguka wakati wakipasha misuli moto kabla ya mechi yao ya ligi daraja la pili, klabu yake ya Durban City imesema.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipelekwa hospitali kabla ya mechi ya Durban dhidi ya Milford FC na mchezo huo ukasimamishwa baada ya kipindi cha kwanza waamuzi walipopewa taarifa kuwa Zondi amefariki.

Chanzo cha kifo chake hakijajulikana.

"Ni kwa masikitiko makubwa sana tunathibitisha kifo cha Sinamandla Zondi, almaarufu Sgora, mchezaji anayependwa sana miongoni mwa jamii ya Durban City," klabu hiyo ilisema katika taarifa.

Faraja kipindi hiki kigumu

"Sinamandla alikuwa zaidi ya mchezaji mwenye kipaji, alikuwa anashirikiana na wenzake vizuri, rafiki, kaka, na mtoto na aliwahamasisha wote wale waliomfahamu.

"Tunawakumbuka na kutowa salamu zetu za rambirambi kwa familia yake, marafiki, wachezaji wenzake, makocha na yeyote aliyeguswa na msiba huu. Tutaendelea kuwafariji wale walio karibu na yeye katika kipindi hiki kigumu."

Mchezaji huyo wa safu ya ulinzi alianza kucheza soka la kulipwa Septemba 2021 na msimu huu amekuwa akicheza mechi nyingi akiwa na timu yake ambayo kwa sasa inaongoza jedwali la msimamo na wanajiandaa kupanda daraja hadi katika ligi kuu ya Afrika Kusini.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#