Sport
Dollar
38,3143
0.02 %Euro
43,6230
0.43 %Gram Gold
4.095,4000
-0.09 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Raia wengi wa kigeni wanapitia nchi hiyo kwa lengo la kuanza safari ya hatari kupitia Bahari ya Shamu kwa kutumia maboti yaliyojaa kupitiliza.
Siku ya Jumatano Djibouti imesema itaanza kuwarejesha makwao "wahamiaji haramu" na kuwataka waondoke nchini humo kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili.
Raia wengi wa kigeni wanapitia nchi hiyo kwa lengo la kuanza safari ya hatari kupitia Bahari ya Shamu kwa kutumia maboti yaliyojaa kupitiliza.
Mwaka 2024, watu wasiopungua 558 walifariki wakati wakijaribu kuvuka bahari,hii ni kulingana na Umoja wa Mataifa.
Wizara ya Mambo ya ndani tayari "imewaomba walio katika nchi yetu kinyume cha sheria kuondoka" kufikia mwisho wa mwezi Aprili, Alexis Mohamed, mshauri wa Rais Ismael Omar Guelleh, ameiambia AFP, bila ya kusema ni raia wangapi wa kigeni.
Safari ya hatari
Uamuzi huu ni kushughulikia masuala "ya usalama na afya," Mohamed alisema.
Taifa hilo lililoko katika mwambao wa pwani ni moja kati ya mataifa yenye raia wachache barani Afrika ikiwa na kama watu milioni moja, na linajulikana kwa kuwa na utulivu katika eneo ambalo halina usalama wa kutosha.
Iko kilomita 26 tu kutoka Yemen kupitia mkondo wa Bab-el-Mandeb.
Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji -- wengi kutoka nchi jirani ya Ethiopia -- hukabiliana na hali ngumu ya kuvuka bahari hiyo ili kuepuka vita, majanga asilia na hali mbaya ya uchumi.
Wengi hujaribu kufika Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Kiarabu ambapo wanaweza kupata kazi kama vibarua au wafanyakazi wa ndani.
Comments
No comments Yet
Comment