Dollar

38,3196

0.02 %

Euro

43,5942

0.36 %

Gram Gold

4.091,3200

-0.19 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Washukiwa hao wanne wamekiri makosa yao wiki iliyopita baada ya mamlaka kuwakamata wakiwa na siafu 5,000.

Wabelgiji, Mvietnam,Mkenya waliopatikana na siafu, kuhukumiwa mwezi ujao

Watu wanne wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefikishwa katika mahakama nchini Kenya Jumatano wakishtumiwa kujaribu kusafirisha maelfu ya siafu walio hai kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kuwa na aina yoyote ya wanyamapori au nyara za serikali bila kibali ni kosa la jinai nchini Kenya, adhabu yake ni faini isiyopungua dola 10,000 na miaka isiyopungua mitano gerezani.

Wabelgiji Lornoy David na Seppe Lodewijckx, wote wana umri wa miaka 18, walikamatwa wakiwa na siafu 5,000 wakiwa ndani ya vifuko 2,244 katika Kaunti ya Nakuru, karibu kilomita 160 kutoka mji mkuu wa Nairobi.

Duh Hung Nguyen raia wa Vietnam na Mkenya Dennis Nganga walikamatwa katika kesi nyingine tofauti nchini Kenya, lakini wote wanashtakiwa kwa pamoja.

Aina tofauti ya siafu

Nguyen na Nganga walipatikana na siafu ndani ya mabomba 140 ya sindano wakiwa wamefunikwa kwa pamba, kulingana na nyaraka za kesi ambazo shirika la habari la AFP limefanikiwa kuziona.

Miongoni mwa wadudu hao ni aina fulani ambayo inapatikana tu eneo hilo, na wachunguzi wanasema namna walivyohifadhiwa kunaweza kuwafanya wabaki kuwa hai kwa hadi miezi miwili.

Polisi wanakadiria bei ya wadudu huenda ikawa karibu dola 7,700.

David na Lodewijckx walikiri makosa yao ya kuwa na wadudu hao wiki iliopita lakini siyo kwa lengo la kuwasafirisha nje ya nchi, hii ni kulingana na wakili wao Halima Magairo.

Soko la wanyama wa kufugwa nyumbani

"Hawa ni vijana wadogo... na wanajaribu tu kuangalia soko liko vipi na huwezi ukawalaumu kwa kujaribu," Magairo aliiambia AFP baada ya kusikizwa kwa kesi hiyo hivi karibuni.

Mkenya na raia wa Vietnam pia walikiri makosa ya kuwa na wadudu, na wote watahukumiwa tarehe 7 Mei.

Shirika la usimamizi wa Wanyamapori nchini Kenya (KWS) liliwasilisha kesi dhidi ya wanaume hao, likisema "siyo tu uhalifu wa wanyamapori bali pia ni ulanguzi wa wadudu ambao hawapatikani sehemu zingine".

Washukiwa ‘‘walikuwa na nia ya kusafirisha wadudu nje ya nchi ili kuwauza kwa bei ya juu kwa ajili ya kufugwa nyumbani katika masoko ya bara Ulaya na Asia, ambapo kuna uhitaji mkubwa wa aina ya kipekee ya wadudu," KWS ilisema katika taarifa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#