Dollar

38,4187

0.2 %

Euro

43,6380

-0.31 %

Gram Gold

4.062,2800

-1.63 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Viongozi hao wawili watajadili kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya serikali ya Trump kusitisha misaada ya fedha kwa Afrika Kusini na kumtimua balozi wao.

Rais wa Afrika Kusini Ramaphosa kukutana na Trump 'karibuni' kusuluhisha matatizo yao

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Alhamisi kuwa amezungumza na Rais Donald Trump na wanapanga kukutana "karibuni" baada ya uhusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani kuwa na matatizo mwaka huu.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, Ramaphosa alisema yeye na Trump wamekubaliana kuhusu "umuhimu wa kuimarisha uhusiano mwema kati ya mataifa hayo mawili."

"Sote tumekubaliana kukutana karibuni na kujadili masuala kadhaa kuhusu Marekani na Afrika Kusini," alisema.

Trump ameshtumu sera kadhaa za Afrika Kusini za nyumbani na kimataifa, ikiwemo kesi waliowasilisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu vita vya Israel huko Gaza.

Kutimuliwa kwa balozi

Hali hii ya taharuki ilisababisha kutimuliwa kwa balozi wa Afrika Kusini kutoka nchini Marekani mwezi uliopita.

Trump pia alisitisha misaada ya kifedha kwa kile alichokiita sera ya ardhi inayokandamiza wazungu na kuwapa fursa ya ukimbizi wazungu wa Afrika Kusini walio wachache ambao anadai wanateswa.

Ramaphosa alikuwa mwenyeji wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky siku ya Alhamisi ambaye alikuwa Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi. Zelensky alilazimika kukatiza ziara yake hiyo baada ya shambulizi baya la Urusi jijini Kyiv usiku.

Zelensky alisema kupitia mtandao wa kijamii kuwa "atarejea Ukraine mara moja" baada ya kukutana na Ramaphosa, kufuatia mashambulizi ya usiku yaliyosababisha vifo vya watu tisa katika mji huo mkuu wa Ukraine.

‘Vifo’

Ramaphosa anasema alikubaliana na mwenzake wa Marekani kuwa vita hivyo vimalizike.

"Nimezungumza na Rais Donald Trump kujadili kuhusu mchakato wa amani wa Ukraine," alisema.

Viongozi "walikubaliana kuwa vita hivi vimalizike haraka iwezekanavyo ili kusitisha vifo vinavyoweza kuepukika," Ramaphosa alisema kwenye ujumbe huo kwa njia ya mtandao.

Siku ya Jumatatu, Ramaphosa alizungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin na wote wawili wakaahidi kufanya kazi pamoja kwa lengo la kutafuta ‘‘suluhu ya amani" kwa mzozo wa Ukraine

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#