Dollar

38,4292

0.2 %

Euro

43,8350

-0.02 %

Gram Gold

4.095,0600

-0.84 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Brice Oligui Nguema alipata 94.85% ya kura ikilinganishwa na mpinzani wake mkuu, Alain-Claude By-Nze, aliyepata 3.11%, kulingana na matokeo rasmi ya mwisho.

Mahakama ya Gabon yamthibitisha kiongozi wa kijeshi  Nguema mshindi rasmi wa uchaguzi wa urais

Mahakama ya Katiba ya Gabon ilithibitisha siku ya Ijumaa kuwa Rais wa mpito Brice Oligui Nguema ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi huu.

Nguema alipata 94.85% ya kura ikilinganishwa na mpinzani wake mkuu, aliyekuwa waziri mkuu katika serikali iliyoondolewa madarakani ya Rais Ali Bongo, Alain-Claude Bilie-By-Nze, aliyepata 3.11% ya kura, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na Mahakama ya Katiba.

Kura za Nguema zimeongezeka kwa karibu 5% zaidi ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa awali na Wizara ya Mambo ya ndani siku moja baada ya uchaguzi.

Pia kura za By-Nze, ziliongezeka kidogo kutoka 3.02% ya matokeo yaliyotangazwa awali.

Muhula wa Miaka saba

Mahakama imesema watu 642,632 walipiga kura katika uchaguzi huo ambao waliojisajili ni 916,625.

Idadi ya walioshiriki kwenye uchaguzi huo ilikuwa 70.11%.

Wagombea wanane walishiriki kwenye uchaguzi wa urais wa Aprili 12, ambao ni wa kwanza tangu kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi bila umwagikaji wa damu 2023.

Katiba mpya ya Gabon, ambayo ilianza kutumika baada ya kura ya maoni ya mwaka jana, inaruhusu muhula mmoja wa urais kuwa miaka saba na anaweza kutetea kiti chake mara moja tu.

Nguema, 50, aliongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon Agosti 2023 yaliyomuondoa madarakani rais wa zamani Bongo, na kumaliza utawala wa miaka 56 wa familia ya Bongo katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati inayozalisha mafuta.

Nguema alifanya kampeni chini wa muungano wa ‘Rally of Builders’, ambao ulipata kuungwa mkono na vyama kadhaa vya kisiasa pamoja na mashirikisho.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#