Dollar

38,0121

0.09 %

Euro

41,6401

0.41 %

Gram Gold

3.676,7400

0.97 %

Quarter Gold

6.187,2600

0 %

Silver

36,9700

0.52 %

Avraham Neguise aliondolewa kwenye mkutano baada ya mataifa wanachama kukataa kushiriki kwenye kongamano na yeye akiwepo

Balozi wa Israeli atimuliwa katika mkutano wa mauaji ya kimbari ya Rwanda

Balozi wa Israeli nchini Ethiopia Avraham Neguise alitimuliwa katika mkutano kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda ulioandaliwa na Umoja wa Afrika siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje imesema kuwa Neguise ameondolewa baada ya nchi wanachama kukataa kushiriki kwenye kongamano pamoja naye.

Wizara hiyo pia imeshtumu taarifa za Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Youssouf, wakati wa hafla hiyo.

“Ni jambo la kusikitisha sana kwamba hafla ya kuwakumbuka Watutsi waliouawa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda, ambapo balozi wa Israeli nchini Ethiopia alikuwa amealikwa, [Youssouf] aliamua kuleta siasa za kupinga Israeli,” ilisema taarifa hiyo.

Mwezi Julai 2021, Israeli ilisema imejiunga tena na Umoja wa Afrika kwa nafasi ya mwanachama muangalizi.

Neguise, ambaye ni mbunge wa zamani wa chama cha Likud, amekuwa balozi wa Israeli nchini Ethiopia tangu mwezi Agosti 2024.

Mwezi Februari 2023, mwanadiplomasia wa Israeli alifukuzwa kwenye mkutano wa 36 wa viongozi wa nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa.

Tukio hili linakuja huku jeshi la Israeli likiendeleza mashambulizi yake mengine Gaza tangu Machi 18 na tangu wakati huo vikosi vyake vimewaua watu zaidi ya 1,400, na kuwajeruhi zaidi ya 3,400, na kuweka kikomo kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ya Januari pamoja na kubadilishana wafungwa katika eneo hilo.

Zaidi ya Wapalestina 50,700 wameuawa Gaza tangu Israeli kuanza mashambulizi ya kikatili Oktoba 2023, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mwezi Novemba mahakama ya Kimataifa ya ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu Gaza.

Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika mahakama ya kimataifa ya haki (ICJ) kwa kuendeleza vita kwenye eneo hilo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#