Sport
Dollar
38,0249
0.1 %Euro
41,9913
0.65 %Gram Gold
3.647,7500
0.18 %Quarter Gold
6.187,2600
0 %Silver
36,7600
-0.03 %Jamaa za watu 155 waliofariki kwenye ajali walikuwa wameishtaki Boeing kati ya Aprili 2019 na Machi 2021 kwa vifo, uzembe na madai mengine.
Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing imefikia makubaliano yatakayowaepusha kushtakiwa, kesi ambayo ilikuwa imepangwa kuanza Jumatatu kutokana na ajali ya shirika la Ethiopia 2019 ya ndege hiyo aina ya 737 MAX iliowaua watu wote waliokuwemo ndani, wakili wa waliowasilisha kesi alisema.
Kesi hiyo iliyokuwa ifanyike Chicago ilikuwa iwe na walalamikaji wawili waliopoteza jamaa zao kwenye ajali hiyo, lakini mashauri yote mawili yalifikiwa makubaliano Jumapili jioni, kampuni ya wanasheria ya Clifford law imeiambia shirika la AFP.
Ndege hiyo ya Boeing ilianguka 10 Machi, 2019, dakika sita tu baada ya kupaa kutoka mji wa Addis Ababa kwa safari ya kuelekea Kenya, na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo ndani.
Jamaa za watu 155 walikuwa wameishtaki Boeing kati ya Aprili 2019 na Machi 2021 kwa vifo, uzembe na madai mengine.
Uwezekano wa kesi
Kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita, kulikuwa na kesi 18 dhidi ya Boeing, mtu anayefahamu zaidi kuhusu shauri hili ameiambia AFP.
Makubaliano ya Jumapili yanamaanisha kuwa kesi zingine nne zaidi zimefikiwa maelewano tangu wakati huo, vyanzo zaidi vya mahakama viliiambia AFP.
Jaji wa Marekani Jorge Alonso amegawanya kesi hizo za Boeing katika makundi ya walalamikaji watano au sita, akifuta tu kesi pale alipojiridhisha kuwa mashauri yote yamefikiwa makubaliano.
Mwezi Novemba, watengenezaji hao wa ndege waliafikiana na familia ya mwanamke mmoja aliyefariki kwenye ajali hiyo.
Ajali ya Indonesia
Ajali ya shirika la ndege la Ethiopia ilifwatwa na ajali nyingine iliyohusisha ndege aina ya MAX plane - ya Lion Air iliyoanguka nchini Indonesia Oktoba 2018, na kuwaua watu wote 189 waliokuwemo ndani.
Boeing pia ilikabiliwa na kesi kadhaa kutoka kwa familia za waliokufa kwenye ajali hiyo ya Lion Air. Ni kesi moja tu ambayo bado ilikuwa haijafutwa, kufikia mwishoni mwa mwezi Machi.
Makubaliano hayo ya Boeing na walalamikaji yamekuwa ni ya siri.
Kampuni hii ya kutengeneza ndege ya Marekani "imekiri makosa hadharani kwa ajali zilizohusisha ndege aina ya MAX kutokana na mfumo wake wa MCAS... uliochangia kwa mikasa hiyo," wakili alisema alipofika mbele ya kamati ya uchunguzi mwezi Oktoba.
Mfumo huo wa MCAS ulisemekana kuwa na hitilafu katika ajali zote mbili za ndege ya Ethiopia na Lion Air.
Kusimamishwa kwa ndege
Mkasa huo ulisabababisha kuwe na vikao maalumu vya bunge la congress, huku wabunge waliokuwa na hasira wakitaka kupata majibu, na kufanyika kwa mabadiliko katika uongozi wa kampuni hiyo. Ndege zote aina ya 737 MAX zilisimamishwa kwa zaidi ya miezi 20.
Baadaye Boeing ilibadilisha mfumo wake wa MCAS chini ya uangalizi wa shirika la kuratibu safari za ndege la Marekani, ambalo hatimae lilitoa idhini kwa ndege hizo kuanza tena huduma zake mwezi Novemba 2020.
Makubaliano haya ya sasa ya Boeing pia huenda yakakabiliwa na kesi nyingine ya jinai katika mahakama moja huko Texas mwezi Juni kuhusu ndege aina ya MAX.
Kesi hiyo inatokana na shauri moja la mwezi Januari 2021 lililoahirishwa kati ya Boeing na Wizara ya Sheria kuhusu ajali hizo mbili za ndege aina ya MAX.
Mwezi Mei 2024, Wizara ya Sheria ilifahamisha mahakama kuwa kampuni ya Boeing imekiuka masharti ya makubaliano. Hii ilikuwa baada ya tukio la Januari 2024 ambapo ndege ya shirika la Alaska ya 737 MAX ililazimika kutuwa kwa dharura kutokana na sehemu ya ndege kupeperushwa na upepo.
Mwezi uliopita Jaji wa Marekani Reed O'Connor aliagiza kufanyike kesi ya jinai Juni 23 baada ya kufuta makubaliano ya awali kati ya Boeing na Wizara wa Sheria.
Comments
No comments Yet
Comment