Dollar

38,0150

0.08 %

Euro

41,8191

0.7 %

Gram Gold

3.669,3900

0.77 %

Quarter Gold

6.187,2600

0 %

Silver

36,8900

0.31 %

Rais Felix Tshisekedi ametakiwa kujibu maswali kuhusu miundombinu mibovu na mazingira mabaya ya usafi katika maeneo ya mji mkuu.

Rais wa DRC akabiliwa na hasira za raia alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa na mafuriko

Siku ya Jumatatu rais wa DRC Felix Tshisekedi alikutana na wananchi waliokuwa na hasira ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu wasiopungua 33 katika mji mkuu Kinshasa.

Mafuriko huwa na athari mbaya mjini Kinshasa, mji ambao uko kwenye kingo za mto Congo, ulio wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya mto Nile.

Mifumo mibovu ya majitaka yamesababisha kuziba kwa mitaro ambapo pia wakazi hutupa taka katika maeneo wanaoishi watu wa kipato cha chini.

Wale wanaoishi katika mabanda na mitaa ambayo haijawekewa mipango sahihi wako katika hatari zaidi kwenye mji ambao una idadi ya watu kupita kiasi, ukikadiriwa kuwa na watu milioni 17.

‘Mungu awalinde’

"Baba, umewaacha watoto wako barabarani," mkazi mmoja alimwambia Tshisekedi, ambaye yeye pamoja na mke wake Denise Nyakeru waliwatembelea watu karibu 600 waliopata hifadhi kwenye uwanja wa michezo ambao umegeuzwa na kuwa sehemu ya makazi ya muda.

"Wanakuita mwamba lakini husaidii watu wako," mkazi mmoja alimwambia, akimuita kwa jina lake la utani kwa Kifaransa.

Kiongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pia alikabiliwa na maswali kuhusu miundombinu mibovu na mazingira mabaya ya usafi katika maeneo ya mji mkuu.

"Uwe na afya njema na Mungu akulinde," Tshisekedi alisema, akiwa amezingirwa na walinzi wa rais, kabla ya kuondoka kwenye uwanja huo.

Magari yarejea barabarani

Watu wasiopungua 33 wamefariki kutokana na mafuriko hayo ya hivi karibuni na karibu 50 wamelazwa hospitalini, hii ni kulingana na wizara ya mambo ya ndani.

Karibu familia 5,000 zimeathiriwa, Waziri wa Afya Samuel-Roger Kamba amewaambia waandishi wa habari.

Siku ya Jumatatu, maji ambayo yalikuwa yamezamisha barabara kuu ya kuelekea uwanja wa ndege hapo awali yalianza kupungua, na magari yakaanza kurejea barabarani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#