Sport
Dollar
38,4292
0.2 %Euro
43,8350
-0.02 %Gram Gold
4.095,0600
-0.84 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mgodi wa Niou unatarajiwa kupata tani 20.22 ya dhahabu katika kipindi cha zaidi ya miaka minane, maafisa wamesema
Burkina Faso imewapa leseni ya mradi wa dhahabu kampuni ya uchimbaji madini ya Urusi Nordgold, serikali hiyo ya Afrika Magharibi imesema, ikilenga kupata fedha kutokana na bei kubwa ya dhahabu ili kuimarisha uchumi uliodorora kwa sababu ya ukosefu wa usalama.
Hatua hii inaashiria uhusiano mkubwa wa kiuchumi kati ya Urusi na Burkina Faso, wakati utawala wa kijeshi uliopindua serikali 2022 ukiendelea kujitenga na washirika waliozoeleka wa Magharibi na kujiweka karibu na Urusi.
Mgodi wa madini ya dhahabu wa Niou, uliopo katika mkoa wa Kourweogo eneo la Plateau ya kati huko Burkina Faso, uko kwenye eneo la kilomita mraba 52.8 kwenye sehemu ambayo leseni yake ya uchimbaji iko kwa jina la Jilbey Burkina, na sasa mmiliki wa kampuni hiyo ni Nordgold. Nordgold tayari inafanya shughuli zake za uchimbaji katika migodi ya Bissa na Bouly.
Siku ya Alhamisi baraza la mawaziri lilisema kuwa mgodi wa Niou unatarajiwa kuzalisha karibu tani 20.22 za dhahabu katika kipindi cha zaidi ya miaka minane.
Sheria mpya za uchimbaji madini
Kampuni ya Jilbey Burkina itabaki na hisa za 85% katika mradi huo, huku serikali ya Burkina Faso ikiwa na hisa 15% bila kuchangia mtaji wowote, kwa mujibu wa sheria mpya za uchimbaji madini nchini humo.
Mradi huu utachangia dola milioni 89 katika bajeti ya serikali kipindi ambacho watakuwa wanachimba, baraza la mawaziri lilisema.
Bei ya dhahabu imepanda kwa zaidi ya 25% mwaka huu, ikichangiwa na ukosefu wa usalama na sera za biashara za Rais wa Marekani Donald Trump.
Burkina Faso, ambayo imekuwa ikikabiliana na wapiganaji tangu 2015, ni mzalishaji mkubwa wa madini ya dhahabu. Kulingana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Swissaid, ambalo hufanyia tathmini masuala ya uchimbaji madini, nchi hiyo ilizalisha zaidi ya tani 57 mwaka 2023.
Wachimbaji wadogo
Makampuni yanayoendesha uchimbaji wa madini ya dhahabu huko ni pamoja na IAMGOLD ya Canada na Endeavour Mining, pamoja na kampuni ya Australia, West African Resources.
"Ushirikiano na kampuni ya Nordgold na wachimbaji wengine ni muhimu (kwa serikali ya Burkina Faso) wakati nchi ikikabiliwa na upungufu wa fedha za bajeti," amesema Ulf Laessing, mkuu wa masuala ya Sahel katika shirika la Kijerumani la Wakfu wa Konrad Adenauer.
Hata hivyo, mradi wa Niou utakuwa kwenye eneo lenye wachimbaji wengi wadogo na huenda ukawanyima wachimbaji wadogo wadogo kipato muhimu, alisema.
Serikali inasema mgodi huo unaweza kutoa ajira kwa watu 204, wakati huohuo ukisaidia kulinda ajira za watu katika mgodi wa karibu wa kampuni ya Bissa Gold SA.
Comments
No comments Yet
Comment