Dollar

38,4292

0.2 %

Euro

43,8350

-0.02 %

Gram Gold

4.095,0600

-0.84 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Israel imeendeleza mauaji ya kimbari kw alengo la kunyakua ardshi ya Wapalestina n akuwahamisha kwa lazima

Jeshi la Israel laamuru Wapalestina zaidi kuhamishwa hadi Magharibi mwa Gaza

Jeshi la Israel lilitoa maagizo zaidi ya kuwahamisha Wapalestina huku kukiwa na mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo lililozingirwa, na hivyo kuzidisha hali ya kibinadamu.

Msemaji wa jeshi Avichay Adraee alichapisha taarifa juu ya X na maonyo ya kuhamishwa kwa wale walioko mashariki mwa Jiji la Gaza, pamoja na Al-Jadeedah, Al-Turkman na kitongoji cha kaskazini mashariki mwa Zeitoun.

Shambulio laua makumi ya Wapalestina

Wanne wauawa, 30 wakitoweka chini ya vifusi baada ya shambulio la Israel - waokoaji Shirika la ulinzi wa raia wa Palestina katika eneo lililozingirwa la Gaza limesema shambulizi la Israel katika mji wa Gaza liliua watu wanne na kuwaacha "zaidi ya 30" wanaohofiwa kuzikwa chini ya vifusi vya nyumba.

"Wahudumu wetu waliweza kuwaokoa mashahidi wanne na majeruhi watano kufuatia shambulio hilo," alisema msemaji wa ulinzi wa raia Mahmud Bassal, akiongeza kuwa "zaidi ya watu 30" wanadhaniwa kupotea chini ya vifusi na "wahudumu wetu hawawezi kuwafikia kwa sababu ya ukosefu wa mashine muhimu".

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#