Sport
Dollar
38,4292
0.2 %Euro
43,8350
-0.02 %Gram Gold
4.095,0600
-0.84 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Msaidizi mwandamizi wa Rais wa Ukraine amesema mashambulizi hayo kwa raia sharti yasitishwe.
Takriban watu tisa wameuawa na zaidi ya 60 kujeruhiwa katika shambulizi ‘kubwa’ lililofanyika katika mji wa Kiev siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa huduma ya dharura ya taifa ya Ukraine, na kuongeza kuwa, shambulio hilo ni kubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza kwa mapigano.
Mamlaka nchini Ukraine zilitoa tahadhari ya shambulio, na mwandishi wa habari za AFP alisikia mlipuko mkubwa katika mji huo.
“Urusi imeanzisha mashambulizi Kiev,” imesema huduma ya dharura kupitia mtandao wa Telegram, ikionyesha idadi ya vifo.
“Kwa mujibu wa takwimu za awali, watu tisa wameuawa na 63 kujeruhiwa,” imesema, na kuongeza kwamba, miongoni mwao, 42 wapo hospitali, sita kati ya wakiwa ni watoto.
Wilaya tano katika mji mkuu zimepata athari, ikiwemo moto ambao tayari umezimwa katika majengo ya serikali.
Serikali pia imesema shambulio hilo pia limeharibu makazi ya watu.
“Utafutaji wa watu chini vya vifusi unaendelea,” imesema.
Baadhi ya wananchi walikusanyika chini ya majengo baada ya tahadhari kutolewa, ameshuhudia mwandishi wa habari wa AFP.
Mara ya mwisho Kiev kushambuliwa kwa makombora ilikuwa ni mwezi Aprili ambapo takriban watu watatu walijeruhiwa. Imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi ya hapa na pale tangu Urusi ilipoanzisha mashambulizi ya moja kwa moja Februari, 2022.
Mashariki mwa Ukraine, mji wa Kharkiv ulishambuliwa na makombora saba mwanzoni mwa Alhamisi, Meya wa Mji Igor Terekhov amesema.
Comments
No comments Yet
Comment