Sport
Dollar
38,1220
0.08 %Euro
43,5645
0.98 %Gram Gold
4.016,0000
1.54 %Quarter Gold
6.511,6500
0 %Silver
39,7700
0.45 %Mazoezi haya yanaratibiwa kwa pamoja na Jeshi la Wanamaji la India na lile la Tanzania na yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
India na mataifa kadhaa ya Afrika wameanza mazoezi ya pamoja katika pwani ya mji wa Dar es Salam nchini Tanzania, ikiashiria hatua kubwa katika ushirikiano katika eneo la ulinzi kati ya India na Afrika.
Zoezi hilo la siku sita chini ya mpango wa AIKEYME lilizinduliwa siku ya Jumapili na linaratibiwa kwa pamoja na Jeshi na la Wanamaji la India na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Limejumuisha washiriki kutoka mataifa 10 ya Afrika ikiwemo Visiwa vya Comoro, Djibouti, Kenya, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Ushelisheli, Afrika Kusini, India na nchi wenyeji, Tanzania.
“Zoezi hili linaashiria dhamira yetu ya pamoja ya kuhakikisha usalama na amani katika eneo la Bahari ya Hindi,” amesema afisa mmoja wa Jeshi la Wanamaji la India katika taarifa.
“Inaonesha uwezo wetu wa kukabiliana na tishio katika bahari pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.”
‘Mwanzo mpya’
Meli za kijeshi za India INS Chennai (uwezo wa kuharibu makombora), INS Kesari (kwa ajili ya vifaru kutuwa) na INS Sunayna (ya doria baharini) ni miongoni mwa zile zinazotumika kwenye mazoezi hayo, ikiwa ni moja ya dira za usalama za India na ukuaji kwa wote katika kanda (SAGAR).
Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Stergomena Lawrence Tax, ambaye alikuwa mwenyeji mwenza wa hafla ya ufunguzi wakiwa ndani ya meli ya INS Chennai, aliitaja hatua hii ya mazoezi ya pamoja kama “mwanzo mpya” katika ushirikiano wa kimkakati wa masuala ya bahari kati ya Afrika na India.
“Katika wakati huu ambao mambo yanabadilika sana. ushirikiano wa kikanda siyo tena jambo la hiari— ni lazima,” Tax aliambia waandishi wa habari. “Zoezi hili linatusaidia sisi kufanya mazoezi pamoja, kupanga pamoja na kushirikiana pale panapohitajika. Tunaona fahari kuwa sehemu ya historia hii.”
Miongoni mwa mambo watakayoshirikiana ni upangaji wa majukumu, mazoezi ya kuendesha kituo cha kuratibu shughuli wakiangazia operesheni dhidi ya uharamia na mazoezi ya pamoja ya namna ya kuingia kwenye meli na kufanya msako.
Ujuzi wa hali ya juu
Michezo na utamaduni pia ni miongoni mwa mambo yaliyopangwa ili kuimarisha utashi miongoni mwa washiriki.
“Ushirikiano huu ni muhimu katika kujenga uaminifu,” alisema Tax. “Inaonesha dunia kuwa Afrika na India wako sako kwa bako kuweka usalama katika bahari yetu.”
Kuanzia Aprili 16-18, hatua ya mazoezi ya baharini ya AIKEYME itaanza, yakiangazia mazoezi ya doria katika bahari, operesheni na uokoaji kwa kutumia ujuzi wa hali ya juu.
Tanzania, ambayo ni moja ya nchi yenye sehemu kubwa ya bahari Afrika Mashariki, inalichukulia zoezi hili kwa umuhimu mkubwa katika kuimarisha uwezo wake wa kukabiliana na uharamia, uvuvi haramu na uhamiaji haramu katika bahari yake.
“Tumeona namna vitisho vya usalama katika bahari vinavyotatiza uchumi wetu. Kupitia mazoezi haya ya AIKEYME, tutapata ujuzi wa hali ya juu wa kulinda pwani yetu na kushirikiana na wengine kwa wakati ufaao,” Tax aliliambia shirika la habari la Anadolu.
Ushirikiano zaidi
Mazoezi haya chini ya mpango wa AIKEYME pia yanaenda sanjari na mpango wa India wa kuimarisha usalama na ukuaji katika kanda zote ulioanzishwa na Waziri Mkuu Narendra Modi kwa lengo la kuzidisha ushirikiano wa kimkakati na washirika wake wa bara la Afrika.
Kwa Tanzania, ushirikiano huu ni zaidi ya faida za kijeshi.
“Hii ni hatua ya mwanzo katika kuleta ushirikiano zaidi wa usalama baharini, biashara na kukabiliana na majanga,” alisema Tax. “Inathibitisha imani yetu kwamba Bahari ya Hindi inatakiwa kuwa eneo la amani na mafanikio kwa wote.”
Comments
No comments Yet
Comment