Sport
Dollar
38,2564
0.07 %Euro
44,0773
-0.13 %Gram Gold
1.157,1500
-2.11 %Quarter Gold
6.947,4100
0 %Silver
40,2000
0.07 %Marekani inaandaa mpango wa kufunga ofisi za ubalozi nchini Eritrea, Gambia, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lesotho, na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kulingana na mapendekezo.
Marekani inapunguza shughuli zake za ubalozi barani Afrika, na kusababisha hali ya wasiwasi kuhusu mustakbali wa kuimarisha masuala ya afya, elimu, na uchumi.
Chini ya utawala wa Trump, taarifa za agizo la rais zilizoonekana zinadhihirisha mipango ya kufanya mabadiliko katika Idara ya Afrika na kupunguza shughuli za shirika la misaada la USAID.
Marekani, ambayo kwa kawaida imekuwa na mtandao mkubwa wa ofisi za ubalozi barani Afrika — ikiwa ya pili baada ya China—inapanga kufunga balozi zake nchini Eritrea, Gambia, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lesotho, na Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na ubalozi mdogo nchini Cameroon na Afrika Kusini.
Mapendekezo ya muswada yanaonesha kuwa wana nia ya kufunga Idara ya kusimamia masuala ya Afrika, inayoshughulikia masuala ya kuimarisha demokrasia, haki za binadamu, sera ya wakimbizi, usawa wa jinsia, na masuala ya tabianchi.
Kusitisha misaada
Tangu mwezi Januari, Marekani imesitisha misaada kwa shirika la USAID kwa siku 90.
Kusitishwa kwa misaada kumetatiza miradi ya afya zaidi, elimu, na maendeleo Kusini mwa jangwa la Sahara, kama vile tiba za kufubaza virusi vya UKIMWI, kujilinda dhidi ya malaria, huduma ya afya kwa kina mama wajawazito, na misaada katika sekta ya kilimo.
Nchi kama Kenya, Uganda, na Nigeria zimelazimika kusitisha au kuondoa kabisa miradi ya kusaidia kuokoa maisha ya watu.
Shirika la USAID linasema sasa linaelekeza juhudi zake kwa ‘‘nchi za kimkakati’’, na kuondosha shughuli zake maeneo mengine.
Kulingana na takwimu za Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani, nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo Guinea ya Ikweta, Eritrea, Gabon, Guinea-Bissau, Mauritius, Sao Tome na Principe, na Ushelisheli, hazijapata msaada wowote mwaka huu.
Nyingine ni, Cape Verde, visiwa vya Comoro, na Gambia, zilipata msaada kidogo tu.
Suluhu ya nyumbani
Baadhi ya serikali za Afrika, zinatafuta suluhu ya nyumbani. Nigeria imetenga dola milioni 200 kujaza pengo kwa misaada ya huduma za afya.
Hata hivyo, nchi nyingi bado zinakabiliana na changamoto kama ufisadi na misingi dhaifu ya utawala bora, kuzifanya iwe vigumu kuendeleza juhudi hizo.
Wataalamu wanaonya hadi pale mataifa ya Afrika yatakapokuwa na washirika tofauti wa kimataifa na kutumia raslimali zao za nyumbani vizuri, itakuwa vigumu kuimarisha sekta ya afya na hatua zote zilizopigwa huenda zikarejeshwa nyuma.
Comments
No comments Yet
Comment