Sport
Dollar
38,2869
0.04 %Euro
43,4084
-0.71 %Gram Gold
4.053,9300
-2.57 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kumekuwepo na ongezeko la mapigano katika eneo hilo katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kati ya wakulima na wafugaji
Watu wasiopungua 11 wameuawa katika mashambulizi ya wafugaji waliokuwa na silaha katika kijiji cha Afia, eneo la Ukum, jimbo la Benue, kaskazini kati mwa Nigeria.
Tukio hili limetokea siku tano tu baada ya kuuawa kwa wakulima zaidi ya 50 katika jimbo hilo.
Kulingana na Iyorkyaa Kaave, kiongozi wa kijiji kilichoshambuliwa, shambulizi la Jumanne mchana “lilipangwa kwa lengo la kuondoa wakulima wazawa.”
“Shambulizi la leo kwa kijiji cha Afia lilikuwa la kikatili, kwa kuwa waliokuwa na silaha walishambulia kijiji, kuwafyatulia wakazi risasi na kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo, na wengine wengi kujeruhiwa,” alisema.
Katika miezi michache iliyopita kanda ya kaskazini kati mwa Nigeria kumekuwa na ongezeko la mapigano kati ya wakulima na wafugaji. Mashambulizi hayo katika jamii zote kwenye eneo hilo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 100 katika kipindi cha wiki mbili.
Mapigano kati ya wakulima na wafugaji nchini Nigeria yamekuwa moja kati ya changamoto kubwa katika miaka ya hivi karibuni. Chanzo ikiwa ni kugombania ardhi na maeneo ya maji pamoja na kuzuia njia za kupita mifugo, uwizi wa mifugo, na uharibifu wa mimea.
Wakati msemaji wa polisi wa jimbo la Benue Sewuese Anene akisema juhudi zinaendelea kurejesha hali ya usalama katika kijiji cha Afia, wakazi wanamtaka Rais Bola Tinubu kuchukua hatua madhubuti, wakionya kuhusu hatua yoyote ya kutaka kufanya majadiliano na wale waliohusika katika mauaji hayo.
Comments
No comments Yet
Comment