Sport
Dollar
38,1191
0.08 %Euro
43,6157
1.06 %Gram Gold
4.009,0200
1.36 %Quarter Gold
6.511,6500
0 %Silver
39,7400
0.36 %Jamii iliyoshambuliwa imekuwa ikikabiliwa na matukio ya vurugu katika wiki za hivi karibuni
Watu zaidi ya 40 wameuawa katika uvamizi wa usiku wa manane kwenye kijiji cha Zike eneo la Bassa, Jimbo la Plateau, huku machafuko yanayofanywa na makundi yenye silaha yakiendelea eneo la kaskazini-kati mwa Nigeria.
Shambulio hilo, lililoanza saa sita usiku wa kuamkia Jumatatu, liliendelea kwa karibu saa mbili, hii ni kulingana na vyanzo tofauti vilivyozungumza na shirika la habari la Anadolu.
Huku ikiwa zaidi ya watu 40 wamethibitishwa kuuawa, karibu wakazi 1,000 wamekimbia makazi yao, kulingana na Joseph Chudu Yonkpa, katibu mwenezi wa taifa wa shirika la vijana la Irigwe.
Yonkpa aliongeza kuwa waliojeruhiwa walikuwa walikuwa wanatibiwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Jos na vituo vya karibu vya afya.
Alfred Alubo, msemaji wa polisi katika Jimbo la Plateau, alithibitisha tukio hilo lakini akasema idadi kamili ya waliouawa bado haijulikani. Alisema taarifa rasmi itatolewa pale tu maelezo zaidi yatakapopatikana.
Jamii ya eneo la Zike imekabiliwa na mashambulio katika wiki za hivi karibuni, huku watu zaidi ya 20 wakiuawa katika matukio tofauti kabla ya shambulio la hivi sasa.
“Hatuko salama. Tunahitaji msaada wa serikali na maafisa wa usalama. Ukatili unaofanywa na wapiganaji hawa ni zaidi ya uvamizi na mauaji,” alisema mkazi mmoja Peter Mba.
Licha ya kutembelewa na Mkuu wa Majeshi ya nchi kavu ya Nigeria Olufemi Oluyede na mshauri wa usalama Nuhu Ribadu -- ambao wote waliahidi kuimarisha hali ya usalama -- mashambulio yameendelea kote katika Jimbo la Plateau.
Comments
No comments Yet
Comment